Rouhani: Kujitokeza wananchi kwa wingi katika uchaguzi kumemfelisha adui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i71428-rouhani_kujitokeza_wananchi_kwa_wingi_katika_uchaguzi_kumemfelisha_adui
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi kumepelekea taifa la Iran lipate ushindi katika kukabiliana na maadui.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Jun 19, 2021 03:46 UTC
  • Rais Rouhani
    Rais Rouhani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi kumepelekea taifa la Iran lipate ushindi katika kukabiliana na maadui.

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo katika ujumbe alioutuma Jumamosi ambapo amewashukuru wananchi wa kujitokeza kwa wingi kaika uchaguzi. Amesema kujitokeza wananchi katika zoezi la upigaji kura jana ni ishara kuwa wanafungamana na malengo matakatifu ya Imam Khomeini MA na pia  wameitikia wito wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Rouhani amesema vita vya kisaikolojia vya maadui si tu kuwa havikuzuia wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura bali pia ni sababu ya kupoteza matumaini maadui na wasiolitakia mema taifa la Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameshukuru wananchi wa Iran kwa kuwa na subira wakati wa vita vya kiuchumi na mashinikizo ya kidhalmu ya adui. Rais Rouhani amesema rais mteule atakuwa na jukumu nzito la kutumia uwezo wote wa nchi ili kuweza kutekeleza matakwa ya wananchi. 

Seyyed Ebrahim Raeisi

Zaidi ya Wairani milioni 59 waliokuwa wametimiza masharti ya kupiga  jana walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa rais ambao ulikuwa wa wagombea wanne baada ya Wagombea wengine watatu kujiondoa katika mchuano huo Jumatano.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Seyyed Ebrahim Raeisi amepata ushindi wa kishindo uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.