Mar 11, 2022 11:50 UTC
  • Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran akosoa ubaguzi wa nchi za Magharibi katika kadhia ya Ukraine

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amekosoa sera za kibaguzi za nchi za Magharibi za kuwatambua wazugu na watu weupe kutoka Ukraine kuwa ndio boza zaidi ya watu wa rangi nyingine na kusema hilo ni doa jeusi na la kufedhehesha.

Hujjatul Islam Kazem Seddiqi amezikosoa Marekani na Magharibi kwa ujumla kwa kutochukua hatua katika vita vya Yemen, Palestina na Syria na kuuliwa watu katika nchi hizo, na kwa kuchukua msimamo mkali kuhusu vita vya Russia nchini Ukraine.

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa: "Kuwepo Iran nchini Syria na Lebanon na uungaji mkono wake madhubuti kwa Wapalestina wanaodhulumiwa, ni kwa sababu vita kati ya Israel na Palestina na vita kati ya Yemen na muungano wa vita unaoongozwa na Saudi Arabia ni vita baina ya haki na batili."

Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesisitiza kuwa, Iran inapinga vita, uharibifu wa miundombinu na mauaji na kusema: "Vita vya Russia na Ukraine ni kinyume na maslahi."

Hujjatul Islam Seddiqi amesema: Marekani na nchi za Magharibi zimefedheheka tena katika vita vya Ukraine mbele ya macho ya walimwengu; nchi hizo hazikuchukua msimamo wa kuwatetea wanaodhulumiwa katika vita vya Yemen  na huko Palestina, uvamizi wa Marekani nchini Syria na kuendelea uporaji wa rasilimali za nchi hiyo, lakini sasa matarumbeta yao yanapaza sauti kuhusu vita vya Ukraine. 

Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameeleza kuwa, hali ya sasa ya kimataifa inaonyesha kwamba ustawi na maendeleo haviwezi kupatikana bila ya kuwepo usalama, na kwamba nchi zote zinahitajiana. 

Katika sehemu nyingine ya hotuba zake za Swala ya Ijumaa, Hujjatul Islam Seddiqi amezungumzia uwezo wa ndani nchi na vijana wanasayansi wa Iran na kusema: "Kuwaamini wanasayansi na vijana wanamapinduzi kunazidisha ari ya maendeleo; na vijana wa nchi hii watatatua matatizo ya vita kamili vya kiuchumi vya ulimwengu wa Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Tags