Larijani asisitiza kuendelezwa ushirikiano wa kistratejia kati ya Iran na Syria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i8779-larijani_asisitiza_kuendelezwa_ushirikiano_wa_kistratejia_kati_ya_iran_na_syria
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe wa pongezi Bi Hadiyeh Khalaf al Abbas Spika Mpya wa kwanza mwanamke wa bunge la Syria na kueleza kuwa stratejia ya Iran ni kushirikiana pande zote na serikali na wananchi wa Syria ili kurejesha amani na uthabiti nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 08, 2016 14:18 UTC
  • Larijani asisitiza kuendelezwa ushirikiano wa kistratejia kati ya Iran na Syria

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe wa pongezi Bi Hadiyeh Khalaf al Abbas Spika Mpya wa kwanza mwanamke wa bunge la Syria na kueleza kuwa stratejia ya Iran ni kushirikiana pande zote na serikali na wananchi wa Syria ili kurejesha amani na uthabiti nchini humo.

Katika ujumbe wake huo alioutuma hii leo, Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani bunge amempongeza Bi Hadiyeh Khalaf al Abbas kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa bunge la Syria, na kusema anataraji kuwa katika duru ya uongozi wake, uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kibunge kati ya nchi mbili utaimarika kieneo na kimataifa.

Katika ujumbe huo, Larijani amesema anataraji pia kuwa makundi ya kigaidi na kitakfiri yataangamizwa na hatimaye serikali na wananchi wa Syria kupata ushindi. Bi hadiyeh Khalaf al Abbas ambaye ni mwanachama wa Muungano wa Umoja wa Kitaifa wa Syria amechaguliwa kuwa Spika mpya wa bunge la Syria na Najdat Anzour amekuwa Naibu Spika wa bunge hilo jipya la Syria.