Marekani yaendeleza uraibu wake wa vikwazo kwa kuiwekea Iran vikwazo vipya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i94676-marekani_yaendeleza_uraibu_wake_wa_vikwazo_kwa_kuiwekea_iran_vikwazo_vipya
Marekani imeyawekea vikwazo makampuni na meli kadhaa katika kuendeleza muelekeo wake wa kiundumakuwili na sera yake ya mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Mar 03, 2023 04:15 UTC
  • Marekani yaendeleza uraibu wake wa vikwazo kwa kuiwekea Iran vikwazo vipya

Marekani imeyawekea vikwazo makampuni na meli kadhaa katika kuendeleza muelekeo wake wa kiundumakuwili na sera yake ya mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika mwendelezo wa malengo yake ya kiuadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutoa msukumo kwa vita vyake vya mchanganyiko na vya kiuchumi dhidi ya taifa la Iran, serikali ya Marekani imeweka vikwazo kadhaa kwa visingizio mbalimbali na kuyalazimisha makampuni ya Kimarekani na mengine yaliyoko katika nchi za tatu kutekeleza vikwazo hivyo.
Maafisa wa serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani wamekuwa wakikiri mara kwa mara kushindwa sera ya mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini kivitendo wanaendelea kufuata siasa hizo hizo kwa sababu vikwazo katika siasa za Marekani daima vimekuwa chombo cha kufanikishia malengo yake ya kujichukukulia maamuzi na hatua za upande mmoja.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Iran IRNA, siku ya Alkhamisi, Wizara ya Fedha ya Marekani iliyawekakwenye orodha yake ya vikwazo  makampuni sita yenye makao yao makuu Iran, Muungano wa Falme za Kiarabu UAE, China na Vietnam pamoja na meli 20 kwa kisingizio cha kuwa na uhusiano na Iran.

Marekani inajulikana kama nchi inayoongoza duniani kwa uwekaji vikwazo, ikiwa na rekodi ndefu zaidi ya kuziwekea nchi zingine kila aina ya vikwazo kwa ajili ya kufanikisha malengo na maslahi yake.../