-
China yalaani vita dhidi ya Iran, yataka usitishaji kamili wa mapigano
May 07, 2026 08:03China imemkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, kwa mazungumzo mjini Beijing, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, akivitaja vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran kuwa “visivyo halali” na kutoa wito wa kusitishwa kabisa kwa mapigano.
-
Iran imewasilisha nyaraka kuhusu jinai za kivita za Marekani na Israel
May 07, 2026 07:53Mkuu wa Shirika la Hilali Nyekundu la Iran amesema wamewasilisha nyaraka 35 zinazoonyesha wazi jinai za kivita zilizofanywa na Marekani na Israel wakati wa mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya Iran, katika taasisi mbalimbali za kimataifa.
-
Pezeshkian: Iran inasimamia nguvu ya Maadili na Uwajibikaji
May 06, 2026 10:58Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran inasimamia nguvu inayojali maadili na uwajibikaji huku akiwatuhumu maadui zake kwa kuwakilisha nguvu zisizo na uwajibikaji.
-
Iravani akanusha vikali azimio la Arab League dhidi ya Iran, asema ni la upendeleo
May 06, 2026 10:43Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amejibu azimio la kikao cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab Legue) dhidi ya Iran kilichofanyika mjini Cairo akisema kuwakingia kifua wavamizi hakuwezi kubadili ukweli wa kisheria.
-
Iran yazindua utaratibu mpya wa kudhibiti meli zinazopita Mlango Bahari wa Hormuz
May 06, 2026 08:07Iran imezindua rasmi mfumo mpya wa udhibiti wa usafiri wa majini katika Mlango Bahari wa Hormuz.
-
Qalibaf: Hali katika Mlango Bahari wa Hormuz imekuwa “isiyovumilika” kwa Marekani
May 06, 2026 07:57Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ameonya kwamba hali inayoendelea katika Mlango Bahari wa Hormuz imekuwa “isiyovumilika” kwa Marekani, huku akisisitiza kuwa Tehran “bado haijaanza hata hatua zake halisi.”
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Matukio ya Hormuz yadhihirisha kuwa suluhisho la kijeshi halipo
May 05, 2026 05:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyed Abbas Araghchi, amesema kuwa matukio ya karibuni katika Mlango wa Bahari wa Hormuz yameweka wazi tena kwamba hakuna suluhisho la kijeshi kwa mgogoro wa kisiasa unaoikumba kanda ya Asia Magharibi, akisisitiza upya sera ya Jamhuri ya Kiislamu ya kufuatilia diplomasia kutoka katika nafasi ya nguvu.
-
Iran yasema “tamaa isiyo na mwisho ya Marekani haina mipaka”
May 05, 2026 05:30Iran imesema kuwa Marekani haijaacha mwenendo wake wa madai kupita kiasi na tamaa isiyo na kikomo, ikithibitisha kuwa imepokea jibu la watawala wa Washington kuhusu pendekezo la Iran la mpango wa pointi 14 unaohusu mazungumzo ya pande zote, yenye lengo la kusitisha vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Meli ya kijeshi ya Marekani yapigwa kwa makombora mawili baada ya kupuuza onyo la Iran
May 04, 2026 11:47Shirika la Habari la Fars limetangaza kuwa, meli ya Jeshi la Wanamaji la Marekani imepigwa kwa makombora mawili baada ya kupuuza onyo la Jeshi la Majini la Iran.
-
Iran yawanyonga magaidi watatu wa Mossad waliopatikana na hatia ya kuwauwa askari usalama katika ghasia za Mashhad
May 04, 2026 10:29Watu watatu waliopatikana na hatia ya kuhusika katika ghasia na machafuko makubwa, mashambulizi dhidi ya askari usalama, na kuwa na uhusiano na Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) wamenyongwa katika mkoa wa Khorasan Razavi, kaskazini mashariki mwa Iran.