-
Iran: Tumeingia katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani kwa nia njema
Feb 16, 2026 23:05Ismail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa Tehran imeingia katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani kwa mtazamo wenye mwelekeo wa matokeo, huku ikibainisha shaka kuhusu taarifa zinazokinzana za Washington.
-
Araghchi, Grossi wakutana Geneva kabla ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na US
Feb 16, 2026 08:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi wamekutana katika jiji la Geneva nchini Uswisi, kabla ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani.
-
Sisitizo la Iran la kuendeleza mazungumzo na kubakisha machaguo yake, kuanzia makombora hadi ufungaji wa Lango-bahari la Hormuz
Feb 16, 2026 07:37Wakati mivutano kati ya Iran na Marekani inazidi kuongezeka, Tehran imesisitiza kuwa, machaguo yake yote yako mezani, licha ya mazungumzo yanayoendelea baina yake na Washington.
-
Iran na Tanzania kupanua ushirikiano wa karantini na kilimo
Feb 16, 2026 06:48Mkuu wa Shirika la Ulinzi wa Mimea la Iran ameeleza azma ya taifa hili ya kukuza ushirikiano na Tanzania katika uga wa karantini na kilimo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran awasili Geneva kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani
Feb 16, 2026 02:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, amewasili katika mji wa Geneva nchini Uswisi kwa ajili ya duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa amani wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Jenerali Mousavi: Mapambano dhidi ya Iran yatakuwa funzo kwa Trump
Feb 16, 2026 00:02Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Donald Trump anapaswa kufahamu kwamba kuingia katika mapambano ya kijeshi na Iran kutakuwa funzo lenye athari kubwa, ambalo matokeo yake yatamzuia kufanya vitisho na majigambo kwenye jukwaa la kimataifa.
-
Iran yaingia kwenye klabu ya mataifa yenye bidhaa za juu za tiba ya seli
Feb 15, 2026 23:29Taasisi ya Utafiti ya Royan Research ya Iran imezindua bidhaa sita mpya zilizotengenezwa ndani ya nchi katika nyanja ya tiba ya seli na uhandisi wa tishu, hatua inayoiweka Iran miongoni mwa mataifa yanayozalisha bidhaa za kisasa za tiba zinazojulikana kama Advanced Therapy Medicinal Products (ATMPs).
-
Sheikh Maher Hammoud: Uvamizi wa kijeshi dhidi ya Iran utawasha moto Asia Magharibi
Feb 15, 2026 08:47Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amesema kuwa, uchokozi wowote mpya dhidi ya Iran utapelekea kuwaka moto katika eneo lote la Asia Magharibi.
-
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Iran: Mpira uko kwenye uwanja wa Marekani kuthibitisha azma ya kufikia makubaliano ya nyuklia
Feb 15, 2026 07:26Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema ni zamu ya Marekani kuonyesha azma ya kufikia makubaliano yanayolenga kutatua suala la nyuklia la Tehran.
-
Araqchi: Sarakasi ya Munich dhidi ya Iran imedhihirisha namna Ulaya ilivyopoteza ushawishi wake wa kijiopolitiki
Feb 15, 2026 04:30Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Mkutano wa Usalama wa Munich uliokua na mtazamo dhidi ya Iran umegeuka na kuwa kongamano la sakarakasi na hivyo kudhihirisha namna Ulaya ilivyopoteza ushawishi wake wa kijiopolitiki na umuhimu wa kistratejia.