Mar 02, 2024 03:06 UTC
  • Masharti ya makundi ya muqawama ya Palestina kuhusu mazungumzo ya kusimamisha vita

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ametoa ufafanuzi kuhusu masharti ya makundi ya muqawama katika mazungumzo ya kusimamisha vita na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika sehemu moja ya ufafanuzi wake, Ismail Hania amesema kuwa, HAMAS imekuwa ikionesha nia ya kutaka makubaliano ya kusimamisha vita na Israel lakini hiyo haina maana kuwa haiko tayari kuendelea na mapambano dhidi ya utawala huo dhalimu.

Mkuu huyo wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS ameongeza kukwa, utawala wa Kizayuni hivi sasa unaendelea kufanya jinai kubwa mno na za kutisha kama mauaji dhidi ya watoto wadogo, wanawake na raia wa kawaida, kuwalazimisha wananchi wa Palestina kuwa wakimbizi na kuwatesa kwa njaa na kiu na mauaji ya kimbari, lakini hilo halijalizuia taifa la Palestina kuendelea na mapambano yake dhidi ya utawala huo katili.

Wanamapambano wa Palestina wametoa vipigo vikali kwa wanajeshi katili na vamizi wa Israel

 

Vile vile amesema: Kwa miezi kadhaa sasa adui Mzayuni amekumbwa na mapambano ya kishujaa ya wananchi na wanamapambano wa Palestina kwenye Ukanda wa Ghaza na amekwama kwenye kinamasi cha Ghaza. Adui huyo aliyezatitiwa kwa silaha za kila namna za mauaji ya umati, anaendelea kufanya jinai za kuua kwa halaiki wanawake na watoto hata vichanga wa Palestina. Adui anaota anapodhani kwamba anaweza kuitoa Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa kwenye maana yake ya asili kwa kuuzingira Msikiti wa al Aqsa na kuwapa silaha walowezi wa Kizayuni ili wafanye mauaji dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi. Inabidi adui atambue kuwa ndoto yake hiyo kamwe haitoaguka.

Mkuu huyo wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, harakati hiyo imekuja na mitazamo miwili kwa kuzingatia hali halisi ilivyo kwenye medani ya mapambano.

Mtazamo wa kwanza ni wa kutambuliwa uwezo na nguvu za makundi ya muqawama na mapambano ya Palestina katika kuendelea kusimama imara kukabiliana na utawala wa Kizayuni na kwamba uhakika huo umejionesha wazi kwenye Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa.

Mtazamo wa pili unahusiana na turufu na nafasi imara na madhubuti waliyo nayo wanamapbmanao wa Palestina hasa kutokana na kushikilia idadi kubwa ya mateka Wazayuni. Suala hilo la mateka wa Kizayuni walioko mikononi mwa makundi ya muqawama ya Palestina ni turufu kwa makundi hayo kwenye mazungumzo ya kusimamisha vita na Wazayuni.

Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS 

Katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, Benjamin Netanyahu na genge lake linalofanya jinai huko Ghaza wamekuwa wakizungumzia mara kwa mara suala la kusimamishwa vita hasa baada ya kudhihirika wazi kuwa jeshi la utawala wa Kizayuni halina uwezo wa kupata ushindi katika vita vya Ghaza wala kuwakomboa mateka wa Kizayuni. Netanyahu na baraza lake la vita la Kizayuni wanajaribu kufunika kushindwa Israel huko Ghaza, kuficha vita na ugomvi mkubwa ndani ya baraza hilo la mawaziri wa serikali ya Netanyahu na pia kujaribu kufifiliza malalalamiko makubwa ya wakazi wa utawala wa Kizayuni kutokana na kufeli vibaya Netanyahu na genge lake.

Malalamiko dhidi ya serikali ya Israel yameongezeka sana hivi sasa ndani ya utawala wa Kizayuni hasa kutokana na kushindwa kukomboa mateka Wazayuni walioko mikononi mwa wanamuqawama wa Palestina. Mpasuko ndani ya serikali ya genge la Netanyahu lenye misimamo mikali ya Kizayuni unazidi kuwa mkubwa siku baada ya siku huku familia za mateka Wazayuni zikiendelea kuilaani serikali yake kwa kuwadanganya na kusema uongo kuhusu mateka hao.

Harakati ya HAMAS ambayo ni mwakilishi mkuu wa Wapalestina katika mazungumzo ya kusimamisha vita inaendelea kutoa msimamo wake kwenye mazungumzo hayo kwa kuzingatia hali hiyo mbaya iliyo nayo serikali ya Benjamin Netanyahu sambamba na uwezo mkubwa walio nao wanamapambano wa Palestina katika vita vinavyozidi kulivunja moyo na kulikatisha tamaa jeshi la Israel. 

 

HAMAS inaendelea na mazungumzo yake pia na viongozi wa nchi mbalimbali za eneo hili sambamba na kuhakikisha kwamba makundi yote ya Palestina yanakuwa na msimamo mmoja kwenye mazungumzo hayo. 

Moja ya mambo ambayo yanaonesha uwezo na nguvu za makundi ya muqawama ya Palestina ni kwamba kamwe hayatowaachilia huru wanajeshi wa Israel inaowashikilia na mabaki ya wanajeshi Wazayuni walioangamizwa, ila baada ya kupata dhamana kamili ya kukomeshwa vita, kuondoka kikamilifu wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kwenye maeneo ya Ukanda wa Ghaza na kuondolewa mzingiro uliowekewa ukanda huo kwa miaka mingi sasa.

Vile vile kila mtu anaelewa jinsi utawala wa Kizayuni usivyoheshimu ahadi hata moja. HAMAS na makundi mengine ya muqawama ya Palestina yanalielewa hilo vyema pengine kuliko mtu mwingine yeyote. Hivyo makundi hayo yako macho kwenye mazungumzo ya kusimamisha vita utawala wa Kizayuni wa Israel, na hata mashrti yao kwenye mazungumzo hayo yanazingatia kikamilifu uhakika huo.

Tags