Idadi ya vifo vya Wazayuni yaongezeka hadi watu 1000
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103242-idadi_ya_vifo_vya_wazayuni_yaongezeka_hadi_watu_1000
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa, idadi ya Wazayuni waliouawa katika operesheni za hivi karibuni za wapiganaji wa muqawama wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu imefikia 1000.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 09, 2023 02:07 UTC
  • Idadi ya vifo vya Wazayuni yaongezeka hadi watu 1000

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa, idadi ya Wazayuni waliouawa katika operesheni za hivi karibuni za wapiganaji wa muqawama wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu imefikia 1000.

Katika kukabiliana na maovu ya utawala wa Kizayuni, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeshambulia ardhi zinazokaliwa kwa mabavu zikiwemo Tel Aviv, Ashdod na Ashkelon kwa mamia ya makombora na maroketi tangu Jumamosi ya tarehe 7 Oktoba.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Fars, gazeti la Kizayuni la Yediot Aharanot limeripoti kuwa, idadi ya Wazayuni waliopoteza maisha katika operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa imefikia watu 1000 na idadi ya watu waliotekwa nyara na vikosi vya Hamas ni zaidi ya watu 150.

Siku ya Jumapili jioni, jeshi la Israel lilitangaza idadi ya vifo vya Wazayuni vilivyotokana na mapigo ya wapiganaji wa muqawama wa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kuwa 700.

Mauaji ya kinyama yanayofanywa na utawala wa kigaidi wa Israel katika Ukanda wa Gaza

Kabla ya hapo, vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni viliripoti kwamba makadirio yanaashiria kuwa, idadi ya mateka wa Kizayuni huko Ghaza ni kati ya watu 150 hadi 200.

Ziyad Al-Nakhleh, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina alitangaza Jumapili jioni kwamba harakati hiyo pekee imewakamata mateka zaidi ya Wazayuni 30.

Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa jeshi la Kizayuni, wapiganaji wa muqawama wa Palestina bado wanapigana na askari wa utawala huo katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Vikosi vya Al-Qassam vilitangaza kuwa wapiganaji wa Hamas waliingia katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu siku ya Jumapili pia.