Raisi katika mazungumzo na Bashar Assad: Nguvu ya mapambano ndio kigezo kikuu
(last modified Sun, 12 Nov 2023 06:39:19 GMT )
Nov 12, 2023 06:39 UTC
  • Raisi katika mazungumzo na Bashar Assad: Nguvu ya mapambano ndio kigezo kikuu

Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Syria wamesisitiza katika mazungumzo yao kuwa nguvu na uwezo wa mapambano ndio kigezo kikuu na cha mwisho kinachopasa kuzingatiwa na Waislamu.

Ebrahim Raisi na  Bashar Assad, marais wa Iran na Syria, pamoja na kushauriana na kujadiliana kuhusiana na hali ya Gaza, wamekubaliana kuwa kigezo cha pekee kitakachoainisha matokeo ya mwisho ni nguvu ya muqawama ambao unaendeleza mapambano kwa nguvu zake zote kwa ajili ya kujilinda. 

Raisi alisisitiza jana Jumamosi katika kikao na Rais Assad wa Syria, pambizoni mwa mkutano wa pamoja wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu uliofanyika kujadili matukio ya Palestina, juu ya haja ya kuchukuliwa uamuzi wa kiutendaji katika uwanja huo. Rais wa Iran alitoa pia mapendekezo matatu muhimu katika kikao cha Riyadh ambayo ni kusimamishwa haraka mashambulizi dhidi ya makazi ya raia, kuondolewa mzingiro wa Gaza na kufikishwa misaada ya kibinadamu kwa wananchi wa ukanda huo.

Marais wa Iran na Syria

Pande mbili hizo pia pamoja na kushauriana na kujadiliana kuhusiana na matukio ya kieneo zimekubaliana kwamba zitaendeleza nguvu na uwezo wa muhimili wa muqwama na kuwa kigezo pekee kitakachoainisha matokeo ya mwisho ni nguvu ya muhimili huo ambao unaendeleza mapambano kwa nguvu zake zote kwa ajili ya kujilinda. 

Rais wa Jamhuri ya Iran aidha amesisitiza katika mazungumzo ya pande mbili suala la misaada na jinsi ya kufikishiwa misaada ya kibinadamu kwa watu wanaodhulumiwa wa Gaza.

Rais Bashar Asad wa Syria naye pamoja na kushukuru mazungumzo ya wazi, yaliyojaa hekima na ya uungaji mkono kwa Gaza ya rais wa Iran katika kikao hicho ametilia mkazo udharura wa kusimamishwa haraka mashambulizi ya Wazayuni na kuanza mwenendo wa kutumwa misaada ya kibinadamu kwa wananchi madhulumu wa Gaza.

 

Tags