Chuki dhidi ya Netanyahu zaongezeka, Wapalestina waendelea kujibu jinai za Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104892-chuki_dhidi_ya_netanyahu_zaongezeka_wapalestina_waendelea_kujibu_jinai_za_wazayuni
Matokeo ya karibuni kabisa ya uchunguzi wa maoni yanaonesha kuwa, chuki na hasira za hata Wazayuni wenyewe zinazidi kuongezeka dhidi ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na umaarufu wa wapinzani wake ndani ya utawala wa Kizayuni unazidi kupanda.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 17, 2023 07:04 UTC
  • Chuki dhidi ya Netanyahu zaongezeka, Wapalestina waendelea kujibu jinai za Wazayuni

Matokeo ya karibuni kabisa ya uchunguzi wa maoni yanaonesha kuwa, chuki na hasira za hata Wazayuni wenyewe zinazidi kuongezeka dhidi ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na umaarufu wa wapinzani wake ndani ya utawala wa Kizayuni unazidi kupanda.

Shirika la habari la IRNA limetangaza habari hiyo leo Ijumaa kwa kulinukuu gazeti la Kizayuni la Maariv likitangaza matokeo ya uchunguzi wa maoni wa karibuni kabisa na kusema kuwa, idadi ya viti vya chama cha Likud cha Benjamin Netanyahu ndani ya bunge la nchi hiyo vimebakia 17 tu wakati ambapo viti vya chama cha mpinzani wake, Benny Gantz ambaye ni waziri wa zamani wa vita wa Israel, vimeongezeka na kufikia 42.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, vyama vya muungano tawala vimepoteza wingi wao wa viti kwenye bunge la Israel na hata vikusanya viti vyao vyote, havizidi 42.

Netanyahu anaongoza jinai kubwa kupindukia dhidi ya watoto na wanawake na vizee wa Ukanda wa Ghaza

 

Hii ni katika hali ambayo, mrengo wa upinzani umezidi kupata umaarufu kiasi kwamba, kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, wapinzani hao wa Netanyahu wamekomba viti 78 kati ya 120 vya bunge la Israel.

Huku hayo yakiripotiwa, duru za habari zimesema kuwa, wanamapambano wa Palestina wameendelea kuvipigwa kwa makombora vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko karibu na Ukanda wa Ghaza.

Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imetangaza kuwa, muqawama wa Palestina leo Ijumaa asubuhi umefanya mashambulizi mengine ya makombora dhidi ya vitongoji hivyo vya walowezi wa Kizayuni.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni navyo vimethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, vitongoji vilivyoko karibu na Ghaza vimeshambuliwa tena kwa makombora na Wapalestina.

Wanamapambano hao wa Palestina wametungua pia droni ya kijasusi ya Israel karibu na eneo la al Zaitun, kama ambavyo Jihadul Islami ya Palestina nayo imetangaza kuwa imeshambulia kwa makombora, zana za kivita za adui Mzayuni katika maeneo ya al Sabra na Tel al Hawa.