Harakati ya Fat'h ya Iraq: Vita dhidi ya Wazayuni ndio kwanza vimeanza
(last modified Sun, 26 Nov 2023 12:03:16 GMT )
Nov 26, 2023 12:03 UTC
  • Harakati ya Fat'h ya Iraq: Vita dhidi ya Wazayuni ndio kwanza vimeanza

Mjumbe wa Muungano wa al Fat'h wa Iraq ameashiria jinsi makundi ya muqawama ya nchi hiyo yanavyoyaunga mkono makundi ya muqawama ya Palestina katika vita vya Ghaza na kusema kuwa, makundi hayo yataendelea kushambulia vituo vya wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Iraq.

Kanali ya Televisheni ya al Maaluma imemnukuu Eid al Hilali akisema hayo na kusisitiza kuwa, vita dhidi ya madola vamizi ya Kizayuni na Marekani ndio kwanza yako katika hatua zake za awali.

Ameongeza kuwa, vita dhidi ya Wazayuni na Wamarekani ndio kwanza vimeanza na vinapiganwa katika medani tofauti kuanzia huko Palestina hadi Lebanon, Yemen na Iraq.

Al Hilali ameongeza kuwa, Marekani na askari wake mpaka hivi sasa wanaogopa bali hawana uwezo na katika siku za usoni pia hawatokuwa na uwezo wa kukabiliana moja kwa moja na muqawama kwenye vita vikuwa katika ukanda huu.

Ameongeza kuwa, Marekani inafanya njama za kutia nguvu uwepo na udhibiti wake wa eneo hili kupitia kushambulia misingi ya kiusalama ya nchi za ukanda huu ikiwemo Iraq, lakini harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq, maarufu kwa jina la al Hashd al Sha'bi, imesimama imara kukabiliana na njama hizo za dola vamizi la Marekani.

Bendera ya Israel

 

Kiongozi huyo mwandamizi wa Muungano wa Fat'h katika Bunge la Iraq ameongeza kuwa, wanajeshi wa Marekani hawana haki ya kufanya shambulizi lolote dhidi ya maeneo ya Iraq.

Mwaka 2003 Marekani iliivamia tena Iraq na tangu mwaka huo hadi hivi sasa inafanya njama za kuidhibiti nchi hiyo na inatumia visingizio tofauti kutia nguvu uwepo wake wa kivamizi nchini humo.

Dola hilo la kibeberu linafanya njama pia za kuingilia masuala yote ya Iraq, lakini wananchi na makundi ya muqawama ya Iraq, muda wote yamekuwa yakivuruga njama hizo za Marekani.

Tags