Vikosi vya Yemen vyashambulia 'kwa mafanikio' meli za US na UK
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i108072-vikosi_vya_yemen_vyashambulia_'kwa_mafanikio'_meli_za_us_na_uk
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Yemen amesema vikosi vya baharini vya nchi hiyo vimeshambulia kwa makombora meli za Marekani na Uingereza katika pwani ya nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2024-02-06T09:13:26+00:00 )
Feb 06, 2024 09:13 UTC
  • Vikosi vya Yemen vyashambulia 'kwa mafanikio' meli za US na UK

Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Yemen amesema vikosi vya baharini vya nchi hiyo vimeshambulia kwa makombora meli za Marekani na Uingereza katika pwani ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema hayo leo Jumanne akiwa mjini Sana'a na kuongeza kuwa: Makombora yetu yamepiga kwa usahihi meli ya mizigo ya Marekani ya Star Nasia na nyingine ya Uingereza yenye jina laMorning Tide katika mai ya Bahari Nyekundu.

Amesema mashambulizi hayo ni jibu kwa chokochoko za Marekani na Uingereza, na amezitaka nchi hizo mbili zisubiri majibu makali zaidi kutoka kwa majeshi ya Yemen kutokana na mashambulizi yao mapya dhidi ya taifa hilo la Kiarabu.

Brigedia Jenerali Saree ameongeza kuwa, operesheni dhidi ya utawala wa Kizayuni zitaendelea hadi pale utawala wa Kizayuni wa Israel utakapokomesha jinai zake dhidi ya Wapalestina wa Gaza.

Jana Jumatatu, ndege za kivita za Marekani na Uingereza kwa mara nyingine zilishambulia maeneo tofauti ya Yemen. Aidha usiku wa kuamkia Jumapili, nchi hizo za kibeberu zilishambulia kwa mabomu maeneo 36 katika nukta 13 za maeneo tofauti ndani ya Yemen. 

Brigedia Jenerali Yahya Saree

Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimesema havitasimamisha mashambulizi yake dhidi ya meli za utawala haramu wa Israel katika maji ya Bahari Nyekundu hadi pale utawala huo haramu utakapokomesha mashambulio yake ya kinyama ya angani na nchi kavu dhidi ya Gaza, ambayo tangu Oktoba 7 hadi sasa yameshateketeza roho za Wapalestina wanaokaribia 30,000.

Mashambulizi mapya ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen ambayo yanafanyika kwa ajili ya kuunga mkono jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza hasa baada ya Yemen kupiga marufuku meli za Israel zisitumie Bahari Nyekundu mpaka Wazayuni wakomeshe jinai zao huko Palestina, yanaendelea kulalamikiwa vikali kote ulimwenguni.