Kuhani wa Kiyahudi ahamasisha Wazayuni wafanye mauaji ya kimbari Ghaza
Kuhani mwanamgambo na mhubiri wa mahubiri ya Kizayuni ya utoaji vitisho, Eliyahu Mali, ametoa wito wa kufanywa mauaji ya kimbari ya Wapalestina waliowekewa mzingiro huko Ghaza, akidai kuwa kufanya hivyo kunaendana na Halakha, yaani sheria ya Kiyahudi.

Kuhani huyo wa Kizayuni ameendelea kusema: "yeyote anayekuja kukuua kwa dhana hii haijumuishi tu kijana wa miaka 16, 18, 20, au 30 ambaye sasa anakunyooshea silaha, lakini pia kizazi kijacho cha [wana wa Ghaza], na wale wanaozaa kizazi kijacho [ yaani wanawake wa Ghaza], kwa sababu kiukweli hakuna tofauti".
Kauli hizo za kiuadui na kigaidi za kiongozi huyo wa kidini wa Kizayuni zinatolewa wakati utawala haramu wa Israel ukiwa tayari umeshaua zaidi ya Wapalestina 30,800 na kujeruhi karibu 73,000 katika vita vyake vya kikatili na vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ghaza.
Israel imeshtakiwa na inashutumiwa kwa mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
Uamuzi wa muda wa mwezi Januari uliotolewa na mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa uliiamuru Tel Aviv isitishe vitendo vya mauaji ya kimbari na kuchukua hatua za kuhakikisha misaada ya kibinadamu inatolewa na kuwafikia raia Wapalestina walioko Ghaza.../