Rabi mkuu wa Wayahudi atishia kuondoka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i109392-rabi_mkuu_wa_wayahudi_atishia_kuondoka_katika_ardhi_zinazokaliwa_kwa_mabavu
Rabi Mkuu wa Wayahudi, Ishaq Yosef, ametishia kuwa wataondoka wote Israel iwapo kabila la Lawi litalazimishwa kujiunga na jeshi la utawala wa Kizayuni.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 11, 2024 22:54 UTC
  • Rabi mkuu wa Wayahudi atishia kuondoka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu

Rabi Mkuu wa Wayahudi, Ishaq Yosef, ametishia kuwa wataondoka wote Israel iwapo kabila la Lawi litalazimishwa kujiunga na jeshi la utawala wa Kizayuni.

Kuhani Ishaq Yosef ameeleza kuwa watu wa kabila la Lawi hawalazimiki kujiunga na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel na kwamba jambo hili halipasi kutekelezwa kwa hali yoyote ile. 

Wakati huo huo Benny Gantz, waziri katika baraza la mawaziri la vita la Israel ameitaja hatua ya Ishaq Yosef, Rabi Mkuu wa Wayahudi ya kutishia kuondoka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel) na sisitizo lake la kutojiunga na jeshi kabila la Lawi kuwa ni maafa ya kimaadili kwa jamii ya Israel na kusema: Watu wote, hata Mayahudi wenye msimamo mikali, wanapasa kuhudumu jeshini katika kipindi hiki kigumu.  

Benny Gantz

Kauli hiyo ya Rabi Mkuu wa Israel imeibua mshtuko mkubwa huko Israel.