Wapalestina elfu 10 wangali chini ya vifusi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i111792-wapalestina_elfu_10_wangali_chini_ya_vifusi
Taasisi ya Ulinzi wa Raia ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa Wapalestina elfu 10 bado wapo chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa katika mashambulizi ya jeshi la Israel.
(last modified 2024-05-15T08:29:49+00:00 )
May 15, 2024 08:29 UTC
  • Wapalestina elfu 10 wangali chini ya vifusi

Taasisi ya Ulinzi wa Raia ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa Wapalestina elfu 10 bado wapo chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa katika mashambulizi ya jeshi la Israel.

Taasisi hiyo ya Ulinzi wa Raia ya Gaza imesisitiza katika taarifa yake kuwa Wapalestina elfu kumi bado wako chini ya vifusi na kwamba jeshi la utawala wa Kizayuni linaendelea kuwashambulia wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na huduma za uokozi. 

Wapalestina bado wako chini ya vifusi Ukanda wa Gaza 

Taasisi hiyo imeeleza kuwa: Utawala wa Kizayuni unaoikalia Quds kwa mabavu unashambulia magari, na vifaa vya taasisi hiyo na hadi sasa jeshi la Israel limewauwa shahidi wafanyakazi 69 wa taasisi hiyo na kujeruhi wengine 250.  

Taasisi ya Ulinzi wa Raia ya Ukanda wa Gaza imelaani mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa kimya cha Umoja wa Mataifa mkabala wa hatua ya Israel ya kuzuia kupatiwa mafuta taasisi hiyo ya ulinzi wa raia ya Gaza ni sawa na kufikia ukomo shughuli za wafanyakazi wa huduma za uokoaji za kibinadamu huko Gaza. 

Wapalestina 35,091 wameuliwa shahidi na wengine 78,827 wamejeruhiwa tangu jeshi la utawala wa Kizayuni lianzishe mashambulizi ya kikatili na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza Oktoba 7 mwaka jana.