Nasrallah: Hizbullah imezuia Lebanon kutumbukia katika mgogoro
Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah , Sayyed Hassan Nasrallah amesema harakati hiyo imeizuia Lebanon kutumbukia katika migogoro inayoendelea sasa Mashariki ya Kati na kwamba jitihada zinahitajika kulinda uthabiti huo.
Akizungumza kwa njia ya televisheni kutoka katika mji wa mashariki mwa Lebanon wa Hermel, Nasrallah amesema usalama unapaswa kuimarisha njdani ya Lebanon ili watu waendelee na maisha ya kawaida na uchumi ustawi.
Katibu Mkuu wa Hizbullah amebainisha wasiwasi wake kuhusu harakati za hivi karibuni za magaidi wakufurishaji katika Bonde la Beqaa na hivyo ametoa wito kwa serikali na wananchi wa Lebanon kuhakikisha usalama unadumishwa katika eneo hilo.
Kwa miezi kadhaa sasa wapiganaji wa Hizbullah wamekuwa wakikabiliana na magaidi wakufurishaji katika Bondo la Beqaa na mwezi Julai Sayyed Nasrallah alisema harakati hayo itahakikisha kuna usalama katika eneo hilo.
Sayyed Nasrallah pia ameelezea matumaini kuwa ukurasa mpya utafunguliwa katika siasa za Lebanon kwa kuteuliwa rais mpya baada ya nchi hiyo kutokuwa na rais kwa muda wa miaka miwili kutokana na mgogoro wa kisiasa.
Inatazamiwa kuwa, Michel Aoun, ambaye amepata himaya ya karibu pande zote za kisiasa, atateuliwa kuwa rais wa Lebanon hivi karibuni.