UN yasisitiza udharura wa kuundwa nchi huru ya Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i25230-un_yasisitiza_udharura_wa_kuundwa_nchi_huru_ya_palestina
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza udharura wa kuundwa nchi huru ya Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 16, 2017 12:25 UTC
  • UN yasisitiza udharura wa kuundwa nchi huru ya Palestina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza udharura wa kuundwa nchi huru ya Palestina.

Antonio Guterres ambaye alikuwa safarini nchini Misri amewaambia waandishi habari mjini Cairo kwamba, kuna udharura wa kuundwa nchi huru ya Palestina kwa mujibu wa maazimio ya kimataifa.

Akiwa mjini Cairo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekutana na kubadilishana mawazo na Rais Abdul Fattah al Sisi wa Misri kuhusu suala la kuundwa nchi huru ya Palestina.

Wazayuni waliivamia ardhi ya Palestina na kuunda dola haramu la Israel mwaka 1948 kwa msaada wa wakoloni wa Kiingereza. 

Guterres na al Sisi

Hadi mwaka 1967 utawala ghasibu wa Israel ulikuwa ukikalia kwa mabavu asilimia 55 ya ardhi zote za Palestina na kila mwaka utawala huo katili umekuwa ukipanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi na kutwaa ardhi zaidi za Palestina.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametilia mkazo udharura wa kudumishwa mapambano dhidi ya ugaidi na kutafutwa suluhisho la kisiasa na migogoro ya Mashriki ya Kati.