Mashambulizi ya anga ya Marekani yaua raia 117 mashariki mwa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29632-mashambulizi_ya_anga_ya_marekani_yaua_raia_117_mashariki_mwa_syria
Mashambulizi ya anga ya Marekani na waitifaki wake yameuawa raia wasiopungua 117 akthari yao wakiwa wawanake na watoto wadogo katika mkoa wa Dayr al-Zawr, mashariki mwa Syria.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
May 26, 2017 09:47 UTC
  • Mashambulizi ya anga ya Marekani yaua raia 117 mashariki mwa Syria

Mashambulizi ya anga ya Marekani na waitifaki wake yameuawa raia wasiopungua 117 akthari yao wakiwa wawanake na watoto wadogo katika mkoa wa Dayr al-Zawr, mashariki mwa Syria.

Kwa mujibu wa shirika linalojiita Syrian Observatory for Human Rights, hujuma hizo za muungano wa kijeshi wa Marekani katika mji wa Mayadin zimepelekea kuuawa raia 117 na wengine wengi wakijeruhiwa, mbali na kuharibiwa kikamilifu miundombinu katika eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa na shirika hilo eti la kutetea haki za binadamu imesema kuwa, watoto wadogo 42 ni miongoni mwa makumi ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo ya anga ya US na waitifaki wake.

Hujuma hii dhidi ya raia wasio na hatia inaonekana kuwa na lengo la kuwapa motisha na kuwashajiisha magaidi wa kitakfiri wa Daesh, waliopata pigo hivi karibuni kutoka jeshi la Syria.

Watoto wadogo, wahanga wakuu wa ukatili wa Marekani nchini Syria

Siku chache zilizopita, mtandao wa habari wa Daesh unaoitwa 'Ofisi ya Kuwaenzi Mashahidi' uliripoti kuwa, wanachama 117 wa kundi hilo wameuawa na jeshi la Syria katika siku chache zilizopita, katika mkoa wa Daraa kusini mwa nchi.

Mapema mwezi huu, Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) ilikiri kuwa ndege za kijeshi za US zilitekeleza shambulizi la anga dhidi ya msikiti mmoja nchini Syria ambapo makumi ya watu waliuawa, magharibi mwa mji wa Aleppo (Halab).