Hizbollah yalaani 'hujuma' ya Jumuiya ya nchi za Kiarabu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i2968-hizbollah_yalaani_'hujuma'_ya_jumuiya_ya_nchi_za_kiarabu
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, imelaani hatua ya hivi karibuni ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuitaja harakati hiyo kuwa "kundi la kigaidi" na kusema uamuzi huo ni sawa na "tangazo la hujuma" kutoka Saudi Arabia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 13, 2016 04:05 UTC
  • Hizbollah yalaani 'hujuma' ya Jumuiya ya nchi za Kiarabu

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, imelaani hatua ya hivi karibuni ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuitaja harakati hiyo kuwa "kundi la kigaidi" na kusema uamuzi huo ni sawa na "tangazo la hujuma" kutoka Saudi Arabia.

Katika taarifa, Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qassim amesema utawala wa Saudia unatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa Hizbullah inatajwa kuwa kundi la kigaidi. Akizungumza mjini Baalbek Lebanon, amesema Saudia imewashinikiza mawaziri wa nje wa nchi za Kiarabu kuchukua maamuzi dhidi ya Hizbullah.

Amesema Saudia inapinga Hizbullah kwa sababu harakati hiyo imeweza kutoa pigo kwa utawala haramu wa Israel sambamba na kutetea Umoja wa Kiislamu na kuwaunga mkono watu wa Yemen, Syria na Iraq ambao wanapata masaibu kutokana na udhalimu wa Saudia.

Ikumbukwe kuwa siku ya Ijumaa, nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiarabu zilitangaza katika kikao chao cha Cairo kuwa eti Hizbullah ni kundi la kigaidi. Uamuzi huo ulipingwa vikali na Algeria, Lebanon na Iraq. Uamuzi huo umekuja wiki moja baada ya Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi kutangaza kuwa eti Hizbullah ni kundi la kigaidi.

Tayari nchi muhimu za Kiarabu kama vile Iraq, Algeria, Lebanon na Syria zimetoa taarifa na kupinga uamuzi huo dhidi ya Hizbullah.