Naim Qassem: Migogoro yote duniani inasababishwa na Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i35329-naim_qassem_migogoro_yote_duniani_inasababishwa_na_marekani
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani ndiyo inayosababisha matatizo na migogoro yote duniani hususan ya eneo la Mashariki ya Kati.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 07, 2017 04:09 UTC
  • Naim Qassem: Migogoro yote duniani inasababishwa na Marekani

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani ndiyo inayosababisha matatizo na migogoro yote duniani hususan ya eneo la Mashariki ya Kati.

Shirika la habari la RASA limemnukuu Sheikh Naim Qassem akisema hayo jana mbele ya wanafunzi wa vyuo vikuu mjini Beirut Lebanon na kusisitiza kuwa, baada ya kushindwa njama zake dhidi ya nchi za Kiislamu, leo hii Marekani imeamua kuendesha mashambulizi yake kupitia vyombo vya habari.

Wanapambano wa harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon

 

Ameashiria namna harakati ya muqawama ilivyo imara katika kukabiliana na Wazayuni maghasibu na magenge ya wakufurishaji yaliyoundwa na Marekani na vibaraka wake na kuongeza kuwa, migogoro ya eneo hili inaweza kutatuliwa tu kwa njia ya muqawama, harakati ya muqawama ambayo imeonesha nguvu zake katika matukio mengi mfululizo na kuibadilisha Lebanon kuwa nchi imara.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Hizbullah ameongeza kuwa, hivi sasa Lebanon imekuwa nchi yenye taathira katika eneo hili kutokana na harakati yake ya muqawama.

Amesema, baadhi ya nchi za Kiarabu na za Magharibi zinafanya vikao na kuwashirikisha baadhi ya viongozi wa Lebanon kama njama za kuivunja nguvu Hizbullah lakini kila anayeshiriki kwenye vikao kama hivyo anapaswa kutambua kuwa, wananchi wa Lebanon daima wako pamoja na muqawama na wanaunga mkono umoja na mshikamano wa nchi yao.