Hizbullah: Lebanon si tonge laini kwa yeyote
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i39847-hizbullah_lebanon_si_tonge_laini_kwa_yeyote
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon, amejibu madai ya hivi karibuni ya Avigdor Lieberman, Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel aliyedai kwamba kisima nambari tisa cha mafuta na gesi ya Lebanon katika Bahari ya Mediterranean ni mali ya Israel na kusema, Lebanon sio tonge laini kwa yeyote yule.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2018 04:11 UTC
  • Hizbullah: Lebanon si tonge laini kwa yeyote

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon, amejibu madai ya hivi karibuni ya Avigdor Lieberman, Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel aliyedai kwamba kisima nambari tisa cha mafuta na gesi ya Lebanon katika Bahari ya Mediterranean ni mali ya Israel na kusema, Lebanon sio tonge laini kwa yeyote yule.

Sheikh Naim Qassim sambamba na kusisitiza kuwa matamshi ya hivi karibuni ya waziri huyo wa vita wa Israel ni ya kupenda kujitanua, amefafanua kuwa, hilo ndilo jibu jepesi ambalo utawala wa Kizayuni unatakiwa kulifahamu. Aidha Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria kuwa Israel inakabiliwa na nguvu ya mihimili mitatu ya Lebanon yaani jeshi, taifa na muqawama na kusema kuwa, silaha za Hizbullah zimeelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Avigdor Lieberman, Waziri wa Vita wa utawala Haramu wa Israel

Hii ni katika hali ambayo awali Saad Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon na Michel Aoun, Rais wa Lebanon hivi karibuni walitoa radiamali kali kuhusiana na matamshi hayo ya Avigdor Lieberman na kusisitiza kuwa, madai hayo hayana msingi wowote na ni ya vitisho dhidi ya taifa hilo la Kiarabu. Maeneo ya mafuta na gesi katika maji ya pwani ya Lebanon yapo katika Bahari ya Mediterranean. Lebanon ina visima 10 vya mafuta na gesi na imepanga katika hatua ya mwanzo ianze kuchimba mafuta katika kisima nambari mbili.

Wanamuqawama wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon ambao wanaitia kiwewe Israel

Kwa mtazamo wa weledi wa mambo, changamoto kubwa inayoikabili Lebanon, ni utawala khabithi wa Israel ambao kwa miaka kadhaa ulianza kuchimba mafuta hayo sambamba na kuendesha operesheni za kuvumbua tena nje ya mipaka ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, lengo kuu likiwa ni kutaka kudhibiti vyanzo vyote vya mafuta vya taifa hilo la Kiarabu