Msuguano katika Uhusiano wa Ufaransa na Saudi Arabia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45168-msuguano_katika_uhusiano_wa_ufaransa_na_saudi_arabia
Emmanuel Macron Rais wa Ufaransa amedai kuwa alikuwa na nafasi muhimu katika utatuzi wa mgogoro wa Lebanon mwaka jana. Aidha amefichua kuwa, Saudi Arabia ilikuwa imemkamata kwa wiki kadhaa Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
May 30, 2018 03:34 UTC
  • Msuguano katika Uhusiano wa Ufaransa na Saudi Arabia

Emmanuel Macron Rais wa Ufaransa amedai kuwa alikuwa na nafasi muhimu katika utatuzi wa mgogoro wa Lebanon mwaka jana. Aidha amefichua kuwa, Saudi Arabia ilikuwa imemkamata kwa wiki kadhaa Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri.

Macron katika kujibu swali la Televisheni ya BFM, kuhusu iwapo sera za kigeni za Ufaransa zimepata mafanikio katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita aliashiria safari ya Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri nchini Saudi Arabia Novemba mwaka jana na hatua isiyo ya kawaida ya kujiuzulu na kukamatwa kwake na kubaini wazi kuwa: "Lazima nikumbushe kuwa, Waziri Mkuu (wa Lebanon) alikuwa amekamatwa kwa wiki kadhaa nchini Saudi Arabia."

Hatua hii ya Macron kufichua kadhia hiyo imewakasirisha sana watawala wa Saudi Arabia. Hii ni kwa sababu wakuu wa Riyadh walikanusha vikali kuwa walikuwa wamemkamata Hariri. Hali kadhalika Hariri mwenyewe pia alikuwa amekanusha kuwa alikamatwa.

Shirika la Habari la Saudi Arabia (SPA) siku ya Jumanne lilinukulu duru katika wizara ya mambo ya nje ya nchi hizo zikipinga matamshi ya Macron na kudai kuwa, eti Saudia inaunga mkono usalama na uthabiti wa Lebanon sambamba na kumhami waziri mkuu wa nchi hiyo. 

Utawala wa Saudi Arabia ulimwita Hariri mjini Riyadh Novemba 4 mwaka 2017 na kumlazimu ajiuzulu ili kwa njia hiyo kuandaa mazingira ya kuibuka mgogoro wa kisiasa nchini Lebanon.

Saad Hariri (kushoto) na Emmanuel Macron

Saudia ilikuwa inalenga kuibia mazingira ya chuki za kisiasa dhidi ya Harakati ya Hizbullah ya Lebanon na kuonyesha kuwa Hariri amejiuzulu kwa sababu ya harakati hiyo. Lakini kutokana na radiamali ya viongozi wa ngazi za juu pamoja na msimamo imara wa Hizbullah, njama hiyo ya Saudia iligonga mwamba.

Weledi wa mambo ya kisiasa wanasema kukamatwa Saada Hariri kuliidhihirishia jamii ya kimataifa uso mchafu wa Saudi Arabia na kuitamblisha nchi hiyo kuwa inayokiuka mapatano ya kimataifa kuhusu jumbe za kidiplomasia na safari za maafisa wa ngazi za juu wa nchi zingine.

Wakati Saad Hariri alipojiuzulu akiwa Saudia, Rais Michel Aoun wa Lebanon alimuita balozi mdogo wa Saudi mjini Beirut na kumtaka awafahamishe watawala wa Riyadh kuwa hatima ya Hariri inapaswa kuwekwa wazi mara moja na arejeshwe nyumbani. Lebanon ilitangaza kuwa kama Saudia haingemruhusu Hariri arejee Beirut, basi ingewasilisha malamikio mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ni kwa msingio huo ndio Saudia ikajipata katika njia panda kwani haikutarajia msimamo imara kama huo kutoka kwa wakuu wa Lebanon.

Kwa hakika safari fupi ya Marcron mjini Riyadh mwezi Novemba  imetajwa kuwa iliyowanusuru watawala wa Saudia na hasa Mohammad Bin Salman, mtawala mwanagenzi ambaye ni mrithi wa ufalme wa Saudia.

Saad Hariri wakati akitoa tangazo la kujiuzulu baada ya kulazimishwa kufanya hivyo na Saudia

Katika safari hiyo Macron alimkinaisha Bin Salman kumuachilia huru Hariri. Aidha akiwa Riyadh, Macron alimualika Hariri kutembelea Paris kabla ya kurejea Lebanon na kwa msingi huo mgogoro uliokuwa ukitokkota ulifika ukingoni.

Hivi sasa Macron amefichua yaliyojiri kati ya Saudi na Lebanon ili kwa njia hiyo ajionyeshe kama mpatanishi aliyefanikiwa na kwa njia hiyo kuishinikiza Saudia imkidhie maslahi yake. Lakini jibu kali la Saudia linaashiria kuwa wakuu wa Riyadh hawajaridhishwa hata kidogo na ufichuzi wa Macron na hivyo uhusiano wa pande hizo mbili uko hatarini.