Hizbullah yaikosoa Saudia kwa kuanzisha uhusiano na Israel
Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amekosoa vikali hatua ya utawala wa Saudi Arabia ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel.
Sheikh Nabiil Qawuq amesema kuanzishwa uhusiano wa Saudi Arabia an Israel ni kosa kubwa zaidi na kwamba kwa kuanzisha uhusiano na utawala huo haramu, utawala wa Saudia umethibitisha kwamba haustahiki kusimamia maeneo matakatifu ya Kiislamu.
Afisa huyo mwanadamizi wa Hizbullah ameashiria pia hatua ya kampuni ya satalaiti ya Nile Sat ya Misri ya kusimamisha matangazo ya televisheni ya al Manar ya Lebanon na kusema: Hatua hiyo haiwezi kuficha kufeli kwa Saudi Arabia huko Yemen wala haitafidia kushindwa kwa watawala wa Riyadh huko Syria.
Uamuzi wa Misri wa kukata matangazo ya televisheni ya al Manar inayomilikiwa na Hizbullah katika satalaiti ya Nile Sat umechukuliwa sambamba na safari ya Mfalme Salman wa Saudia nchini humo.