Israel yawadondoshea mabomu Wapalestina wa Gaza
Kwa mara nyingine tena ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimewadondoshea mabomu Wapalestina kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la Israel leo asubuhi imesema: "Ndege zetu zimelenga maeneo kadhaa ya Gaza, yakiwemo maficho ya wanachama wa Hamas."
Utawala haramu wa Israel unadai kuwa, umetekeleza mashambulizi hayo ya anga kwa ajili ya kulipiza kisasi, baada ya roketi 17 kuvurumishwa kutoka kwenye ukanda huo kuelekea Israel.
Hakuna taarifa zozote zilizotolewa kufikia sasa kuhusu maafa na uharibifu uliosababishwa na hujuma hiyo ya anga ya jeshi katili la Israel.

Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wamekuwa wakifanya maandamano karibu kila Ijumaa, kulaani uporaji na kukaliwa kwa mabavu ardhi zao na utawala ghasibu wa Israel.
Wapalestina zaidi ya 140 wameshauawa shahidi hadi sasa na maelfu ya wengine wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari wa utawala haramu wa Israel, tangu yalipoanza maandamano ya Siku ya Ardhi yaliyopewa jina la "Haki ya Kurejea" yaliyoanza Ijumaa ya Machi 30 katika Ukanda wa Gaza.