Hizbullah Iraq: Kuondoka Marekani syria ni ishara ya kushindwa Washington
(last modified Sun, 23 Dec 2018 01:09:46 GMT )
Dec 23, 2018 01:09 UTC
  • Hizbullah Iraq: Kuondoka Marekani syria ni ishara ya kushindwa Washington

Harakati ya Hizbullah ya Iraq imetangaza kuwa, kuondoka kwa majeshi ya Marekani nchini Syria kuna maana ya kushindwa stratijia za jeshi la nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Hizbullah ya Iraq imeashiria uamuzi wa serikali ya Marekani wa kuondoa majeshi yake katika ardhi ya Syria na kusema: Washington ikisaidiana na Saudi Arabia na Imarati zinataka kuwahamishia wapiganaji wa Daesh katika maeneo mengine lakini njama hiyo pia itashindwa na kufeli.

Taarifa hjiyo imeongeza kuwa, kuwepo kwa majeshi ya Marekani katika maeneo ya magharibi mwa Asia kumezidisha uwezo wa makundi ya kitakfiri na kigaidi katika eneo hilo.

Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 19 Disemba alitangaza kuwa, atalirejesha nyumbani jeshi la nchi hiyo lililoko katika ardhi ya Syria. Uamuzi huo umechukuliwa miaka saba baada ya makundi ya kigaidi kushindwa kuiondoa madarakani serikali halali ya nchi hiyo. 

Kuondoka kwa askari wa Marekani Syria ni ishara ya kushindwa

Kwa kisingizio cha kupambana na makundi ya kigaidi, Marekani ilipeleka majeshi yake nchini Syria bila ya idhini ya serikali ya nchi hiyo. Hatua hiyo ilichukuliwa na Serikali ya Donald Trump licha ya kwamba kiongozi huyo alikiri waziwazi kwamba, serikali ya kabla yake ya Marekani ilihusika katika kuanzishwa makundi ya kigaidi likiwemo kundi la kigaidi la Daesh nchini nchini Syria.  

Tags