Mshauri wa Bashar al-Assad: Wamarekani wamekimbia Syria
(last modified Mon, 24 Dec 2018 02:50:13 GMT )
Dec 24, 2018 02:50 UTC
  • Mshauri wa Bashar al-Assad: Wamarekani wamekimbia Syria

Mshauri wa kisiasa na wa masuala ya habari wa Rais wa Syria amesema kuhusu hatua ya wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo kwamba: Wamarekani wamekimbia, kwa sababu sisi tumesimama imara.

Buthaina Shaaban ameashiria kuondoka askari wa Marekani nchini Syria na kueleza kwamba: Uchambuzi wowote unaojaribu kuwaonyesha waliokimbia kuwa wana nguvu na wako imara ni upinduaji ukweli wa mambo.

Bi Buthaina Shaaban ameongeza kuwa: Baadhi wanafanya kila njia ili kulinda haiba na nguvu za upande ulioshindwa na kuachana na hatua yake ya kinyume cha sheria uliyochukua na wala hawana uthubutu wa kuashiria chochote kuhusu sababu za uwezo na nguvu za upande uliosababisha kushindwa upande huo.

Mnamo siku ya Alkhamisi iliyopita, mamia ya malori yaliyobeba zana za kivita za majeshi ya Marekani yaliondoka kwenye maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa Kikurdi wa Syria kuelekea kivuko cha Simalka katika mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Iraq.

Wanajeshi wa Marekani na zana zao za kivita ndani ya ardhi ya Syria

Baada ya miaka saba na kugonga mwamba njama ya makundi ya kigaidi ya kuiangusha serikali halali ya Syria, tarehe 19 Desemba, Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kuwa karibuni hivi majeshi ya nchi hiyo yataondoka katika ardhi ya Syria.

Marekani imejiingiza kinyume cha sheria katika ardhi ya Syria kwa kisingizio cha kupambana na makundi ya kigaidi, ilhali mara baada ya kuingia madarakani, Trump mwenyewe alikiri kuwa, Washington ndiyo mhusika mkuu wa kuasisiwa makundi ya kigaidi, likiwemo la DAESH (ISIS) nchini Syria.../

Tags