Jan 26, 2019 04:33 UTC
  • Mamia ya wanajeshi wa Marekani na malori 250 yenye silaha waingia Syria

Katika hali ambayo Washington inadai kuwa ina mpango wa kuondoa wanajeshi wake huko Syria; kundi moja linalofahamika kama Kundi la Kutetea Haki za Binadamu la Syria limeripoti habari kuhusu kuwasili nchini humo mamia ya wanajeshi wa Marekani wakiwa na makumi ya malori yenye silaha.

Kinyume na madai ya karibuni ya Rais Donald Trump wa Marekani kwamba amekusudia kuwaondoa huko Syria wanajeshi wa nchi yake; kundi hilo la kutetea haki za binadamu la Syria limetangaza kuwa: Mamia ya wanajeshi wa Marekani  huku wakiwa wameambatana na malori 250 yenye silaha na vifaa vya kilojistiki vya muungano wa Marekani Alhamisi iliyopita katika nyakati za usiku waliwasili katika mikoa ya Halab, Raqqah na al Hasaka huko Syria.  

trump

Rais Donald Trump wa Marekani 
 

Kundi hilo limeongeza kuwa silaha na zana hizo za kijeshi zimegawiwa katika kambi za kijeshi za muungano huo eti wa kupambana na ugaidi unaoongozwa na Marekani katika maeneo ya Ain al Arab, katika uwanja wa ndege wa Ain al Arab, Ain al Issa, Raqqah, Tal Tamir na katika kambi nyingine.  

Tarehe 14 mwezi huu wa Januari kundi hilo la kutetea haki za binadamu la Syria lilitangaza kuwa msafara wa wanajeshi wa Marekani wenye makumi ya magari ya kijeshi umewasili Deir Zor Syria kupitia kivuko kinachounganisha eneo la Furat Mashariki na eneo la Kurdistan la Iraq.  

Tags