Wanamuqawama wa Yemen wavurumisha makombora 4 ya Zilzal-1 kwenye ngome za askari wa Saudia
(last modified Sat, 27 Jul 2019 04:12:45 GMT )
Jul 27, 2019 04:12 UTC
  • Wanamuqawama wa Yemen wavurumisha makombora 4 ya Zilzal-1 kwenye ngome za askari wa Saudia

Jeshi na kamati za wananchi nchini Yemen limevurumisha makombora manne aina ya Zilzal-1 kwenye ngome za vibaraka wa muungano vamizi wa Saudia katika mikoa ya Aseer na Najran kusini mwa Saudia.

Kanali ya televisheni ya al-Masira imekinukuu chanzo kimoja cha jeshi la Yemen kikisema kwamba, makombora matatu aina ya Zilzal-1 yamevurumishwa katika ngome ya askari wa Saudia katika eneo la Abwab Al Hadid ya mkoa wa Aseer ambapo yamewasababishia hasara na uharibifu mkubwa askari wa utawala wa Aal-Saud. Kwa mujibu wa chanzo hicho, jeshi la Yemen kwa kushirikiana na kamati za wananchi, limevurumisha kombora lingine moja aina ya Zilzal-1 katika ngome ya askari wa Aal-Saud katika mkoa wa Najran. Hii ni katika hali ambayo mizinga ya jeshi na kamati za wananchi wa Yemen pia imeyashambulia maeneo ya askari wa Aal-Saud katika eneo la Al Ajashir la mkoa wa Najran ambapo vibaraka kadhaa wa utawala wa Saudia wameangamizwa.

Kombora la zilzal 1

Saudia kwa kushirikiana na Marekani, Imarati na baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu ilianzisha mashambulizi ya kila upande dhidi ya taifa masikini la Yemen mwezi Machi 2015 na kisha kuizingira katika pande tatu za nchi kavu, baharini na angani nchi hiyo. Hadi sasa vita hivyo vya Saudia nchini Yemen vimepelekea kwa akali watu elfu 16 kuuawa na makumi ya maelfu ya wengine kujeruhiwa.

Tags