Marekani yazidi kumimina wanajeshi wake kaskazini mwa Syria + Video
(last modified Sun, 17 Nov 2019 11:23:13 GMT )
Nov 17, 2019 11:23 UTC
  • Marekani yazidi kumimina wanajeshi wake kaskazini mwa Syria + Video

Msafara mwingine mmoja wa wanajeshi wa Marekani umeingia katika mji wa Qamishli mkoani al Hasakah, huko kaskazini mashariki mwa Syria.

Televisheni ya al Alam imetangaza habari hiyo leo na kuongeza kuwa, msafara huo wa wanajeshi wa Marekani umetokea kwenye eneo la Kurdistan la Iraq na kuingia kaskazini mashariki mwa Syria.

Siku tatu nyuma pia, msafara mwingine mmoja wa kijeshi wa Marekani ulivuka mpaka wa Iraq na Syria na kupiga kambi karibu na maeneo yenye visima vya mafuta ya kaskazini mashariki mwa Syria.

Licha ya rais wa Marekani, Donald Trump kudai kuwa ameamua kuondoa wanajeshi wake nchini Syria lakini ametia ulimi puani na sasa misafara ya kijeshi ya Marekani imeanza kurejea kinyume cha sheria huko Syria kwa madai ya kulinda usalama wa visima vya mafuta na eti kuzuia magenge ya kigaidi yasije yakaviteka tena visima hivyo.

Siku chache zilizopita, Rais Bashar al Assad wa Syria aliifananisha Marekani na utawala dhalimu wa Kinazi wa Ujerumani akisema, Washington inaiba waziwazi mafuta ya Syria. Ikumbukwe kuwa Marekani imetuma wanajeshi wake vamizi nchini Syria bila ya idhini ya Umoja wa Mataifa wala ruhusa ya serikali ya nchi hiyo.

Awali maeneo ya mafuta na gesi ya Syria yalikuwa yanakaliwa kwa mabavu na magenge ya kigaidi hasa lile la Daesh (ISIS) kabla ya kuzidiwa nguvu na kutekwa na waasi wa Kikurdi, wapinzani wa serikali halali ya Syria.

Hivi sasa Marekani inatumia mbinu zile zile za magenge ya kigaidi za kuiba mafuta ya Syria na kuyauza nje ya nchi hiyo.

Tags