Israel: Wazayuni kuanza kuitembelea Saudia kwa ziara za 'kidini' na kibiashara
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58758-israel_wazayuni_kuanza_kuitembelea_saudia_kwa_ziara_za_'kidini'_na_kibiashara
Wizara ya Mambo ya Ndani ya utawala haramu wa Israel imesema utawala huo pandikizi utaanza kuwaruhusu Wazayuni kuitembelea Saudi Arabia katika kile kinachotajwa kama safari za kidini na kibiashara.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 26, 2020 09:37 UTC
  • Israel: Wazayuni kuanza kuitembelea Saudia kwa ziara za 'kidini' na kibiashara

Wizara ya Mambo ya Ndani ya utawala haramu wa Israel imesema utawala huo pandikizi utaanza kuwaruhusu Wazayuni kuitembelea Saudi Arabia katika kile kinachotajwa kama safari za kidini na kibiashara.

Tangazo hilo la leo Jumapili la Tel Aviv ni muendelezo wa kuzidi kuwekwa wazi uhusiano wa karibu wa utawala huo wa Kizayuni na nchi za Kiarabu. Aidha kauli hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Israel imetolewa siku chache kabla ya Rais Donald Trump wa Marekani kuzindua 'Muamala wa Karne' ambao unapingwa vikali na Wapestina wenyewe na nchi nyingi duniani.

Ikulu ya White House inatazamia kupata uungaji mkono wa Saudia katika kuzindua na kutekeleza muamala huo ambao Wapalestina wanasema hauna maslahi kwao, bali ni njama za kutaka kuhalalisha jinai za Israel na ukaliaji wa mabavu wa ardhi za Wapalestina na utawala huo ghasibu.

Mrithi wa Ufalme wa Saudia Muhammad Bin Salman (kushoto), Netanyahu na Trump

Baadhi ya nchi za Kiarabu zimekuwa zikifanya juu chini kuboresha uhusiano wao na utawala khabithi wa Israel unaoukalia kwa mabavu mji wa Quds, kilipo kibla cha kwanza cha Waislamu duniani.

Hivi karibuni, ikiwa ni baada ya kupokea mwaliko kutoka Imarati wa kushiriki Maonyesho ya Kibiashara ya Dubai 2020, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema katika taarifa kuwa, "tunawapongeza waandalizi wa maonyesho hayo kwa kuialika Israel, tunakaribisha kwa mikono miwili ushiriki wa Israel katika maonyesho hayo ya Dubai."