Waziri wa Vita wa Israel atoa amri ya kutekwa ardhi zaidi za Wapalestina, Ukingo wa Magharibi
(last modified Tue, 02 Jun 2020 11:30:10 GMT )
Jun 02, 2020 11:30 UTC
  • Waziri wa Vita wa Israel atoa amri ya kutekwa ardhi zaidi za Wapalestina, Ukingo wa Magharibi

Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amemtaka mkuu wa majeshi ya utawala huo katili na ghasibu afanyie uchunguzi njia za kutekeleza kivitendo mpango wa kuteka maeneo zaidi ya Wapalestina ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na aongeze utayari wa jeshi la Israel kwa ajili ya kutekeleza mpango huo.

Gazeti la Kizayuni la Israel Hume limeripoti habari hiyo na kumnukuu waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni, Benny Gantz akisema hayo wakati alipoonana na Aviv Kochavi, mkuu wa majeshi yote ya utawala wa Kizayuni na kuongeza kuwa, kumeundwa timu maalumu ya pamoja ya kufanya uratibu baina ya taasisi na vyombo tofauti kushauriana jinsi ya kutekeleza kivitendo mpango wa kuteka na kuzikalia kwa mabavu ardhi nyingine za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Jana Jumatatu pia, Waziri wa Vita wa Israel alizungumza na kubadilishana mawazo ya  David Friedman, balozi wa Marekani katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kuhusu utekelezaji wa mpango huo wa kuyateka na kuyakalia kwa mabavu maeneo makubwa ya Wapalestina huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wanajeshi wa Israel ni watenda jinai wakubwa

 

Kwa mujibu wa mpango wa kidhulma wa Marekani uliopechikwa jina la "Muamala wa Karne," utawala wa Kizayuni umekusudia kuteka asilimia 30 ya ardhi nyingine za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kutokana na uungaji mkono kamili wa serikali ya Donald Trump. Uporaji huo umepangwa kufanyika tarehe Mosi Julai mwaka huu.

Wakuu na makundi mbalimbali ya Palestina wanasema kuwa, hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa Marekani ulio dhidi ya Palestina uliopachikwa jina la "Muamala wa Karne" na ndio maana viongozi na makundi yote ya Palestina yakawa yanaunga mkono nia ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kuvunja ushirikiano wake na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Tags