Yahya Rasul: Iraq haihitaji askari wa kigeni kwa ajili ya kupambana na ugaidi
(last modified Wed, 03 Jun 2020 07:28:03 GMT )
Jun 03, 2020 07:28 UTC
  • Yahya Rasul: Iraq haihitaji askari wa kigeni kwa ajili ya kupambana na ugaidi

Msemaji wa kamandi kuu ya jeshi la Iraq amesema kuwa, nchi hiyo haihitai askari yeyote wa kigeni kwa ajili ya mapambano na mabaki ya ugaidi.

Rasul aliyasema hayo Jumanne ya jana akibainisha stratijia mpya ya nchi hiyo katika mapambano yake dhidi ya ugaidi na kuongeza kwamba hadi sasa bado kuna magaidi wengi waliosalia katika maeneo tofauti ya Iraq na kwamba maafisa usalama wanakusudia kuanzisha mapambano dhidi ya magaidi hao. Amesema kwamba daghadagha ya maafisa usalama wa Iraq, ni kudhamini usalama wa mipaka ya nchi hiyo na kubainisha kwamba askari na maafisa usalama wa Iraq na kwa kutegemea uwezo wao wa kijeshi na kupitia kupanuliwa ushirikiano wa kiintelejensia litashinda mapambano dhidi ya mabaki ya magaidi hao wa Daesh (ISIS).

Jeshi la Iraq lina uwezo wa kupambana na magaidi, halihitaji msaada wa askari wa kigeni

Kamandi kuu ya jeshi la Iraq ilitangaza jana kuanzisha hatua ya pili ya operesheni iliyopewa jina la 'Mashujaa wa Iraq' kaskazini mwa nchi hiyo. Katika miezi mitatu iliyopita, kiwango cha harakati na uwepo wa magaidi wa Daesh (ISIS) kimeongezeka katika mikoa tofauti ya nchi hiyo ambapo kufikia sasa tayari kumefanyika operesheni kadhaa za kuisafisha mikoa hiyo.

Tags