Abbas akutana na mawaziri wa Israel usiku wa manane Ramallah
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i75384-abbas_akutana_na_mawaziri_wa_israel_usiku_wa_manane_ramallah
Mamhoumd Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amekutana na kufanya mazungumzo na mawaziri wawili wa utawala haramu wa Israel mjini Ramallah, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 04, 2021 08:07 UTC
  • Abbas akutana na mawaziri wa Israel usiku wa manane Ramallah

Mamhoumd Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amekutana na kufanya mazungumzo na mawaziri wawili wa utawala haramu wa Israel mjini Ramallah, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Duru za habari zinaeleza kuwa, Abbas alikutana kwa siri na Nitzan Horowitz, Waziri wa Afya wa utawala wa Kizayuni na mwenzake wa Ushirikiano wa Kieneo, Esawi Freij usiku wa jana Jumapili.

Agosti mwaka huu, Abbas alikutana na kufanya mazungumzo na Benny Gantz, Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS ilisema kitendo cha Mamhoumd Abbas, kukutana na kufanya mazungumzo na Benny Gantz ni sawa na kuwachoma jambia kwa nyuma Wapalestina.

Abbas (kushoto) na Benny Gantz

Hayo yanajiri katika hali ambayo, ushirikiano wa kiusalama na kiuchumi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Israel umeendelea kulalamikiwa vikali na wananchi wa Palestina.

Abbas anaendelea kujikomba kwa Wazayuni katika hali ambayo, Naftali Bennett, Waziri Mkuu wa utawala khabithi wa Israel mwenye misimamo ya kufurutu ada amesisitiza mara kadhaa kuwa, kamwe hatoruhusu kuundwa dola la Palestina katika utawala wake.