Muqawama wa Palestina wafanyia majaribio kombora jipya
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i75616-muqawama_wa_palestina_wafanyia_majaribio_kombora_jipya
Chaneli ya televisheni ya Quds imetangaza kuwa muqawama wa Palestina umefanyia majaribio kombora jipya katika kujizatiti na kuimarisha zaidi nguvu na uwezo wake wa kijeshi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 10, 2021 23:00 UTC
  • Muqawama wa Palestina wafanyia majaribio kombora jipya

Chaneli ya televisheni ya Quds imetangaza kuwa muqawama wa Palestina umefanyia majaribio kombora jipya katika kujizatiti na kuimarisha zaidi nguvu na uwezo wake wa kijeshi.

Kwa mujibu wa chaneli hiyo, muqawama wa Palestina umelifanyia majaribio kombora jipya, ambalo limefyatuliwa kwenye pwani ya Ukanda wa Gaza kuelekea baharini, katika kujizatiti na kuimarisha nguvu na uwezo wake wa kijeshi.

Hayo yanajiri wakati karibu wiki moja nyuma, chaneli ya 12 ya televisheni ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ilidai kuwa, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imefyatua makombora manne ya majaribio kutoka pwani ya Gaza kuelekea baharini.

Mnamo miezi michache iliyopita pia, Fat-hi Hammad, mjumbe mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya Hamas alitangaza kuwa, baada ya kukomeshwa uvamizi wa karibuni wa utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, uundaji makombora mapya ya muqawama umeanza tena.

Hammad amesisitiza kuwa, viwanda na karakhana za Hamas zimeanza tena kazi ya kuunda maelfu ya makombora mengine mapya ili kukomesha chokochoko za utawala wa Kizayuni katika mji wa Baitul Muqaddas.../