Kamanda Msaudi wa ISIS auawa Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i796-kamanda_msaudi_wa_isis_auawa_iraq
Kamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh ameuawa nchini Iraq katika hujuma ya ndege za kivita mkoani Ninevah.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 07, 2016 10:32 UTC
  • Kamanda Msaudi wa ISIS auawa Iraq

Kamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh ameuawa nchini Iraq katika hujuma ya ndege za kivita mkoani Ninevah.

Shobaib Abu Majd al-Kanani, mzaliwa wa Saudi Aarbia, aliuawa pamoja na makamanda wengine wanane wa ISIS Jumamosi usiku.

Aidha siku ya Jumamosi vikosi vya Iraq viliwaua magaidi saba wa ISIS katika hujuma za angani mkoani Kirkuk.

Kwingineko vikosi vya Iraq vimefanikiwa kuwaua magaidi wengine 45 wa ISIS katika mji wa Ramadi mkoani al Anbar.

Leo Jumapili magaidi hao wa ISIS wametekeleza jinai ya kinyama na kuwaua watoto kadhaa mashariki mwa mji wa Ramadi.

Magaidi hao wamekuwa wakitekeleza jinai kaskazini na magharibi mwa Iraq tokea Juni mwaka 2014 walipochukua udhibiti wa baadhi ya maeneo.

Magaidi wa ISIS wamekuwa wakitekeleza jinai dhidi ya watu wa kaumu, madhehebu na dini zote Iraq wakiwemo Waislamu wa madhehebu ya Shia, Sunni, Wakurdi, Wakristo na Waizadi.