Waziri Mkuu wa Israel ajaribu kukwamisha kufufuliwa JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i87380-waziri_mkuu_wa_israel_ajaribu_kukwamisha_kufufuliwa_jcpoa
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ameingiwa na kiwewe kutokana na uwezekano mkubwa wa kufikiwa makubaliano ya kuhuisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA ndani ya siku chache zijazo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 24, 2022 06:20 UTC
  • Waziri Mkuu wa Israel ajaribu kukwamisha kufufuliwa JCPOA

Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ameingiwa na kiwewe kutokana na uwezekano mkubwa wa kufikiwa makubaliano ya kuhuisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA ndani ya siku chache zijazo.

Katika ujumbe wa Twitter, Naftali Bennett amesema, "Natoa mwito kwa Rais wa Marekani Joe Biden, na utawala wa Washington kujizuia, katika dakika hizi za mwisho, kusaini makubaliano na Iran." 

Anadai kuwa, kupasishwa kwa mapatano hayo kutaipa serikal ya Iran robo ya dola trilioni moja, fedha ambazo zitaiwezesha Tehran kuzalisha, kusimika na kuendesha mitambo ya mashinepewa pasi na kizuizi kwa miaka miwili.

Benett ambaye anaonekana kukerwa na ukweli kuwa yumkini mapatano ya kuiondolewa Iran vikwazo vya kidhalimu yatafikiwa karibuni hivi amedai kuwa: Ndani ya mwaka uliopita, tulifanikiwa kuwashawishi wenzetu wa White House wasisalimu amri mbele ya matakwa ya Iran. Tunatumai hali itasalia kuwa hivyo (hata mara hii). Kwa njia moja au nyingine, dola la Israel si mshiriki wa mapatano hayo.   

Mazungumzo ya Viena

Siku chache zilizopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikabidhi kwa mratibu wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo hayo ya kuondolewa taifa la Iran vikwazo, jibu la maandishi la Tehran kuhusiana na nakala rasmi ya rasimu ya mapatano ya Vienna, na sasa inasubiri jibu la Marekani.

Hii ni katika hali ambayo, Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, nchi nyingi duniani zinakubaliana na mapendekezo hayo, lakini bado inasubiriwa Marekani itoe majibu baada ya Iran kutoa majibu ya kimantiki kuhusu mapendekezo hayo ya EU.