Jan 02, 2023 07:13 UTC
  • Jenerali wa Kizayuni akiri kuwa mkakati wa Israel dhidi ya Iran umegonga mwamba

Mkuu wa zamani wa idara ya intelijensia ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kuwa mkakati wa Tel Aviv dhidi ya Iran wa kutegemea vikwazo vikali vya kiuchumi na kuanzisha mpango wa kuzuia hujuma kupitia Marekani umeshindwa.

Meja Jenerali Tamir Hyman, mkuu wa zamani wa idara ya intelijensia ya jeshi la utawala wa Kizayuni amelitahadharisha pia baraza jipya la mawaziri la utawala huo linaloongozwa na Benjamin Netanyahu kwamba stratijia ya hivi sasa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitafika popote.
Jenerali huyo wa Kizayuni amekiri kuwa sera ya vikwazo iliyotekelezwa baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano ya nyuklia ya Iran ya JCPOA haikuifanya Iran itengwe kisiasa na kiuchumi, kwa sababu kutengwa huko hakukuwa na uhalisia na sababu ni kuwa, Tehran inapata uungaji mkono wa kiuchumi wa Russia na China.
Hata hivyo Hyman ameendelea kutoa madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran kwa kusema: "Iwapo Iran itapata bomu la atomiki, kwa mara ya kwanza tutakuwa katika hali ya kuwepo tishio linalohatarisha uwepo wa Israel".
Madai ya afisa huyo wa zamani wa utawala wa Kizayuni yametolewa katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshasisitiza mara kadhaa kwamba uundaji wa bomu hauna nafasi katika kanuni zake za kisiasa.../

 

Tags