-
'Kaa' wa Israel waendelea kuwindwa kwa panga za Muqawama
Sep 10, 2024 07:47Wanamapambano wa kambi ya Muqawama wameendelea kuwashinikiza Wazayuni ili wakomeshe jinai zao dhidi ya watu wa Ghaza kwa kutumia mbinu na njia mbalimbali na kwenye nyuga tofauti ikiwa ni pamoja na kukata mhimili wa kuusaidia utawala wa Kizayuni kwa njia za baharini.
-
Yemen: Jeshi la Majini la Marekani tumelitimua katika Bahari Nyekundu
Sep 10, 2024 07:46Harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Ansarullahi ya Yemen imesema kuwa, imefanikiwa kuwatimua wanajeshi wa Marekani katika Bahari Nyekundu.
-
Mauaji ya kimbari huko Khan Yunis yasababisha zaidi ya mashahidi na majeruhi 100
Sep 10, 2024 04:28Maghasibu wa Kizayuni wamefanya jinai nyingine kwa kuyashamvulia leo Jumanne asubuhi mahema ya wakimbizi huko Khan Yunis katika mkoa wa Al-Mawasi.
-
Jinai za Israel: Watoto 45,000 wa darasa la kwanza wameshindwa kuanza msimu mpya wa masomo Gaza
Sep 10, 2024 01:10Wakati watoto wanajiandaa kwa ajili ya mwaka na siku yao ya kwanza shuleni katika nchi kadhaa za Mashariki ya Kati, takriban watoto 45,000 wenye umri wa miaka sita katika Ukanda wa Gaza wamenyimwa haki hii ya kuanza masomo kutokana na jinai za utawala haramu wa Israel.
-
Kusikika mayowe ya kuunga mkono Palestina barani Ulaya na Marekani
Sep 09, 2024 22:55Mjini London, Paris, Berlin, Geneva, Milan, The Hague, Stockholm, Amsterdam, Oslo na New York, ilishuhudia waandamanaji wakipiga nara dhidi ya utawala katili wa Israel kuunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
-
Takwa la Umoja wa Mataifa la kuwekewa vikwazo Israel
Sep 09, 2024 09:36Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula amesema kuwa, Israel sio tu inazuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza, bali pia inaharibu ardhi na vyanzo vya chakula vya Palestina.
-
Iraq: Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani kuondoa wanajeshi wake huko Iraq katika muda wa miaka 2
Sep 09, 2024 07:18Iraq imesema kuwa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani, ambao ulisalia katika nchi hiyo ya Kiarabu kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh miongo miwili baada ya kuivamia na kuikalia kwa mabavu nchi hiyo mwaka wa 2003, utaondoa kikamilifu wanajeshi wake ndani ya miaka miwili kuanzia sasa. Haya yameelezwa na Thabit al Abbasi Waziri wa Ulinzi wa Iraq.
-
Abu Ubaida: Operesheni ya kivuko cha "Al Karama", imefanywa na mmoja wa mashujaa wa Kimbunga cha Al-Aqsa
Sep 09, 2024 05:44Msemaji wa tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) Abu Ubaida, amebariki operesheni ya kishujaa iliyotekelezwa na mwanamapambano raia wa Jordan Shahidi Maher al-Jazi, katika kivuko cha Karama (Allenby) na kumtaja kuwa ni miongoni mwa mashujaa walioshiriki katika Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa Septemba mwaka jana dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Idadi ya waliouawa shahidi katika Ukanda wa Gaza yafikia 41,000
Sep 09, 2024 03:21Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, idadi ya waliouawa shahidi kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya eneo hilo imefikia 41,000.
-
US yaja na mpango mpya wa kusitisha vita Ghaza, "bila matumaini" ya kufikiwa mwafaka
Sep 09, 2024 03:20Maafisa wa Marekani na wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamesema, Washington "haina matumaini" ya kufikiwa makubaliano ya kubadilishana mateka na makundi ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza, lakini pamoja na hayo, karibuni hivi itawasilisha pendekezo lake jipya.