-
Kuongezeka uwepo kijeshi wa Marekani huko Iraq na Syria
Jan 16, 2024 10:57Marekani ilituma wanajeshi huko Iraq mwaka 2003 wakati ilipoivamia na kuikalia kwa mabavu nchi hiyo mwaka 2003; na kuhusu Syria pia Marekani ilituma wanajeshi wake nchini humo mwaka 2014 kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Kitakfiri la Daesh (ISIS) katika fremu ya Muungano wa Kimataifa wa eti kukabiliana na ugaidi.
-
Yemen yajibu mapigo kwa kuishambulia meli ya mizigo ya Marekani kwa makombora ya balestiki
Jan 16, 2024 03:24Meli ya mizigo inayomilikiwa na Marekani imeshambuliwa kwa kombora la balestiki nje ya pwani ya Yemen, huku wingu la wasiwasi na mvutano mkali likiendelea kutanda katika Bahari Nyekundu kutokana na uungaji mkono usiokoma wa Washington kwa vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Kushtadi mipasuko ya ndani katika utawala wa Kizayuni wa Israel
Jan 16, 2024 03:02Katika hali ambayo, zimepita siku 100 tangu kuanza vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza, vita hivyo vinaonekana kushadidisha migawanyiko na mipasuko ya ndani katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).
-
China yataka kuweko amani jumuishi na athirifu huko Palestina
Jan 15, 2024 23:47Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa China ametoa mwito wa kuwepo amani jumuishi na athirifu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Msemaji wa jeshi la Israel akiri, makombora ya Hizbullah yameuathiri utawala huo
Jan 15, 2024 10:44Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kuwa mashambulizi ya makombora ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon huko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) yamekwua na ufanisi na kulenga shabaha.
-
Sheikh Issa Qassim: Kushiriki Bahrain katika muungano wa baharini wa Marekani dhidi ya Yemen ni "aibu"
Jan 15, 2024 10:19Sheikh Issa Qassim Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain ameitaja hatua ya Manama ya kushiriki katika muungano wa baharini unaoongozwa na Marekani katika Bahari ya Sham dhidi ya Yemen kuwa ni kitendo kibaya, chenye kutia uchungu na cha fedheha.
-
Sheikh Shahriyari: Ni haramu kushirikiana kwa namna yoyote na utawala dhalimu wa Israel
Jan 15, 2024 01:04Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, ni haramu kushirikiana kwa namna yoyote ile na utawala ghasibu wa Israel na kuudhaminia mahitaji yake.
-
Idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa na muqawama yafika 522
Jan 15, 2024 01:04Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kuwa, idadi ya askari wake waliouawa hadi sasa tangu ilipototekelezwa operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa imefikia 522.
-
UN: "Siku 100 za mashambulizi ya Israel huko Gaza zinahisika kama miaka 100" kwa Wapalestina
Jan 15, 2024 01:03Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), amesema siku 100 zilizopita za mashambulizi ya Israel huko Ukanda wa Gaza zimekuwa kama miaka 100 kwa watu wa Gaza.
-
New York Times: Ansarullah bado ina uwezo wa kushambulia meli za Israel
Jan 15, 2024 01:02Gazeti la New York Times limewanukuu maafisa wawili wa kijeshi wa Marekani, wakisema kwamba harakati ya Ansarullah ya Yemen bado ina takriban robo tatu ya uwezo wake wa kurusha makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya meli zinazopita Bahari Nyekundu kuelekea Israel.