-
Misikiti 380 imebomolewa Gaza tangu Israel ianzishe mashambulio ya kinyama Oktoba 2023
Jan 12, 2024 23:19Imeelezwa kuwa, maeneo 383 ya ibada yamebomolewa katika ukanda wa Gaza tangu utawala haramu wa Israel ulipoanzisha mashambulio yake ya kinyama dhidi ya eneo hilo huko Palestina.
-
Muqawama: Tuko pamoja na Yemen, amani haitopakana mpaka Quds ikombolewe
Jan 12, 2024 07:37Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na makundi mbalimbali ya muqawama ya Palestina, Lebanon na Iraq yametoa matamko na kulaani vikali mashamblizi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen na kusisitiza kuwa yako pamoja na wananchi wa Yemen na wataendelea kushirikiana hadi Quds itakapokombolewa.
-
Yemen: Mashambulizi ya US na UK hayatotuzuia kuliunga mkono taifa la Palestina + VIDEO
Jan 12, 2024 07:05Msemaji wa majeshi ya Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Sarii amesema kuwa, mashambulizi ya kiuadui ya Marekani na Uingereza hayatobadilisha msimamo wa Yemen wa kuliunga mkono taifa la Palestina ikiwemo Ghaza na kwamba uadui huo uliofanyika mapema leo Ijumaa dhidi ya Yemen hautoachwa vivi hivi bila ya majibu na kuadhibiwa madola hayo ya kibeberu.
-
Shambulio dhidi ya Yemen, duru mpya ya chokochoko za Marekani na Magharibi katika eneo
Jan 12, 2024 06:00Siku moja baada ya kupitishwa rasimu ya azimio lililopendekezwa na Marekani la kulaani kile kilichoitwa mashambulio ya Yemen dhidi ya meli katika Bahari Nyekundu, Washington imeishambulia Yemen katika duru mpya ya chokochoko zake katika eneo.
-
Ansarullah: Marekani na Uingereza zijiandae 'kulipa gharama kubwa' kwa kuishambulia Yemen
Jan 12, 2024 04:14Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen imezilaani vikali Marekani na Uingereza baada ya kufanya mashambulizi makali dhidi ya vituo vyake ndani ya Yemen, na kuonya kuwa vituo vya kijeshi vya nchi hizo vilivyoko katika eneo vitashambuliwa iwapo zitafanya uchokozi zaidi.
-
US, UK zashambulia vituo vya Ansarullah Yemen kwa sababu ya msimamo wake wa kuwahami Wapalestina
Jan 12, 2024 00:25Marekani na Uingereza zimeshambulia vituo kadhaa vya harakati ya Ansarullah kukabiliana na hatua ya harakati hiyo ya wananchi wa Yemen ya kuzishambulia meli zenye uhusiano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, kwa sababu ya vita vya mauaji ya kimbari na ya halaiki unavyoendesha utawala huo dhalimu dhidi ya Wapalestina wa Gaza.
-
Kiwewe cha Netanyahu cha kufanyika mapinduzi dhidi yake ndani ya chama chake cha Likud
Jan 11, 2024 10:58Waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjami Netanyahu amekumbwa na kiwewe cha kuongezeka hisia za kufanyika mapinduzi dhidi yake ndani ya chama chake cha Likud, jinamizi ambalo amekuwa akifanya kila aina ya jinai ili kulikwepa.
-
Wapalestina wakusanyika katika uwanja wa Mandela Ramallah kuishukuru Afrika Kusini kuhusu kesi ya ICJ
Jan 11, 2024 04:19Wapalestina jana Jumatano walikusanyika katika uwanja wa mwendazake mzee Nelson Mandela huko Ramallah lengo likiwa ni kuishukuru Afrika Kusini kwa hatua yake ya kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya utawala haramu wa Israel.
-
Al Sudani asisitiza kuondoka haraka wanajeshi vamizi wa Marekani huko Iraq
Jan 11, 2024 04:16Waziri Mkuu wa Iraq ameashiria hatua za kuvuruga usalama na amani vya Marekani na kutaka kuondoka nchini humo wanajeshi vamizi wa Marekani haraka iwezekanavyo.
-
Njama za Marekani za kuendelea kubakia kijeshi nchini Iraq
Jan 11, 2024 03:44Licha ya serikali ya Iraq kuitaka Marekani iondoe wanajeshi wake nchini humo, lakini Washington imetangaza kuwa, haina ratiba yoyote ya kutoka katika nchi hiyo ya Kiarabu.