Trump: Obama na Hillary Clinton waliunda kundi la kigaidi la Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/world-i13039-trump_obama_na_hillary_clinton_waliunda_kundi_la_kigaidi_la_daesh
Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump amesema kuwa, Rais Barack Obama na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa nchi hiyo Hillary Clinton ndio walioanzisha kundi la kigaidi la Daesh.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Aug 11, 2016 03:27 UTC
  • Trump: Obama na Hillary Clinton waliunda kundi la kigaidi la Daesh

Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump amesema kuwa, Rais Barack Obama na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa nchi hiyo Hillary Clinton ndio walioanzisha kundi la kigaidi la Daesh.

Trump ambaye jana alikuwa akihitubia wafuasi wake katika mji wa Florida amesema kundi la kigaidi la Daesh linampa heshima maalumu Rais Obama. Donald Trump amesisitiza kuwa Obama na Clinton waliasisi na kuanzisha kundi la Daesh. Amekosoa pia uamuzi wa Rais wa Marekani wa kuondoa jeshi la nchi hiyo nchini Iraq na kuacha nafasi kwa kundi la kigaidi la Daesh. Amesisitiza kuwa Marekani ilipaswa kubakisha baadhi ya majeshi yake katika ardhi ya Iraq ili kutoruhu magaidi waidhibiti ardhi ya nchi hiyo.

Daesh wakikata kichwa cha raia wa Syria

Magaidi wa Daesh ambao wengi wao walipewa mafunzo na shirika la ujasusi la Marekani CIA huko Jordan mwaka 2012 kwa ajili ya kuidhibiti Syria bado wanashikilia maeneo ya Iraq na Syria ambako wanafanya ukatili wa kutisha.