Feb 18, 2016 08:03 UTC
  • Erdogan: Tutawasaka na kuwaadhibu waliotushambulia

Rais wa Uturuki ameahidi kutoa jibu kali kwa watekelezaji wa mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu, Ankara ambapo watu 28 waliuawa hapo jana.

Recep Tayyip Erdogan amesema Uturuki inapata nguvu kubwa ya kukabiliana na maadui wa ndani na nje kila inapochokozwa na kwamba waliotega mabomu mjini Ankara hapo jana watasakwa na kuadhibiwa vikali. Kiongozi huyo amesema nchi yake haitasita kutumia nguvu zake kujilinda.

Jamii ya kimataifa imeungana na Uturuki kulaani hujuma hiyo. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Hossein Jaberi Ansari imelaani tukio hilo na kuahidi kushirikiana na Uturuki katika vita dhidi ya magaidi. Kansela wa Ujerumani. Angela Markel kwa upande wake amesema Berlin inasimama bega kwa bega na Uturuki katika kupambana na watu wenye misimamo mikali na ugaidi.

Mshambulizi ya hapo jana katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara yamesababisha watu 28 kupoteza maisha na zaidi ya 60 kujeruhiwa.

Tags