Marekani yakiri kuuliwa raia katika mashambulizi huko Syria
jeshi la Marekani limekiri kuwa makumi ya raia wameuawa katika mashambulizi ya anga ya ndege za kivita za nchi hiyo huko Syria.
Jeshi la Marekani jana lilitoa taarifa na kukiri kuwa ndege za nchi hiyo limeuwa raia zaidi ya 188 tangu mwaka 2014 hadi sasa katika mashambulizi yaliyofanywa na Marekani kwa kisingiizo cha kupambana na kundi la wanamgambo wa kitakfiri wa Daesh huko Syria.
Kundi kwa jina la "Airways" lenye makao yake Uingereza ambalo hufuatilia na kutoa takwimu za raia wanaouawa katika mashambulizi ya anga limeeleza kuwa, idadi ya raia waliouawa kwenye mashambulizi ya anga huko Syria na Iraq katika kpindi kinachofanana na hicho ni zaidi ya 2100. Taarifa ya jeshi la Marekani imedai kuwa Washington inafanya juhudi kujiepusha na vifo vya raia katika mashambulizi yake ya kijeshi, hata hivyo sehemu ya vifo hivyo haviepukiki.
Mwezi Novemba mwaka jana wa 2016 kulitolewa ripoti mpya 16 kuhusu raia waliouawa katika mashambulizi ya Marekani huko Syria na Iraq. Aidha tarehe 29 mwezi Disemba mwaka jana ndege za kivita za Marekani ziliishambulia na kuisambaratisha gari iliyodaiwa kumilikiwa na Daesh huko kaskazini mwa Iraq; ambapo baadaye viongozi wa Iraq walithibitisha kuwa shambulio hilo lilifanywa katika eneo la kuegeshea magari katika hospitali moja na kwamba waliouawa walikuwa ni raia wa kawaida.