Pyongyang: Komandi ya kijeshi ya askari wa kimataifa mjini Seoul, ivunjwe
https://parstoday.ir/sw/news/world-i31264-pyongyang_komandi_ya_kijeshi_ya_askari_wa_kimataifa_mjini_seoul_ivunjwe
Serikali ya Korea Kasakazini imetoa pendekezo la kuvunjwa kituo kikuu cha kijeshi kwa ajili ya askari wa mataifa tofauti iliyo chini ya Umoja wa Mataifa huko Seoul, mji mkuu wa Korea Kusini ivunjwe.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 03, 2017 04:22 UTC
  • Pyongyang: Komandi ya kijeshi ya askari wa kimataifa mjini Seoul, ivunjwe

Serikali ya Korea Kasakazini imetoa pendekezo la kuvunjwa kituo kikuu cha kijeshi kwa ajili ya askari wa mataifa tofauti iliyo chini ya Umoja wa Mataifa huko Seoul, mji mkuu wa Korea Kusini ivunjwe.

Kituo hicho kwa ajili ya askari wa mataifa tofauti kinachosimamiwa na Umoja wa Mataifa, kilianzishwa mwaka 1950 katika vita ya Korea na hadi sasa kimegeuzwa na kuwa kituo cha vikosi vya Marekani kwa kushirikiana na askari wa kutoka mataifa mengine mjini Seoul ili kuzuia vita vya Korea mbili. Kamisheni ya kitaifa ya usalama nchini Korea Kaskazini imetangaza kuwa, Marekani ilianzisha kituo hicho wakati wa kujiri vita vya Korea mbili kwa ajili ya kuisaidia Korea Kusini.

Askari wa Marekani wakiwasili katika kituo hicho Korea Kusini

Katika ripoti hiyo Pyongyanga pia imesema kuwa, Washington imekusudia kuligeuza eneo la Peninsula ya Korea kuwa suala la dunia kama ambavyo inafanya njama za kukibakisha kituo hicho cha askari wa kimataifa mjini Seoul kwa ajili ya kuendeshea vita baridi katika eneo dhidi ya Pyongyang. Kadhalika Korea Kaskazini imeitaja Marekani kuwa muhusika katika kuchafua usalama na amani sambamba na kuwasha moto wa vita katika eneo hilo. Inafaa kuashiria kuwa, hadi sasa Marekani ina kambi kadhaa za kijeshi nchini Korea Kusini. Uepo wa Washington ndani ya taifa hilo unatajwa na Pyongyang kuwa chanzo cha kuwa tete hali ya eneo la Peninsula ya Korea.

Marekani ikiendelea kujiimarisha kijeshi katika eneo hilo na kuchafua usalama

Washington na Seoul zimekuwa zikiitaka Korea Kaskazini kusimamisha miradi yake ya silaha za nyuklia na makombora yake ya balestiki, suala ambalo limetupiliwa mbali na Pyongyang. Kwa mara kadhaa serikali ya Pyongyang imekuwa ikisisitiza kuwa, vitisho vya Washington ndivyo vinavyochochea mgogoro katika Peninsula ya Korea.