Ndege za kivita za Marekani zaendelea kuua raia Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i32492-ndege_za_kivita_za_marekani_zaendelea_kuua_raia_syria
Raia sita wameuawa na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa mashariki mwa Syria, katika mashambulizi ya ndege za kivita za muungano eti wa kupambana na Daesh (ISIS) unaoongozwa na Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 30, 2017 23:57 UTC
  • Ndege za kivita za Marekani zaendelea kuua raia Syria

Raia sita wameuawa na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa mashariki mwa Syria, katika mashambulizi ya ndege za kivita za muungano eti wa kupambana na Daesh (ISIS) unaoongozwa na Marekani.

Duru za habari zimeliambia shirika rasmi la habari la Syria SANA kuwa, mashambulizi hayo ya jana Jumapili ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na US yalilenga Hospitali ya Aish, maeneo ya al-Nadi na al-Shuhada katika mji wa Abu Kamal, ulioko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Iraq, mkoani Dayr al-Zawr, mashariki mwa Syria. 

Habari zaidi zinasema kuwa, watoto na wanawake ni miongoni mwa raia waliouawa na kujeruhiwa katika hujuma hizo za anga za Marekani na wapambe wake.

Ndege za kivita za Marekani

Mashambulizi ya jana Jumapili yamefanyika siku moja baada ya raia wengine kumi wa Syria kuuawa katika hujuma zingine za muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani, katika kijiji cha Tayibe, mashariki mwa mkoa wa Dayr al-Zawr.

Kwa mujibu kundi linalojiita Syrian Observatory for Human Rights, raia 29 waliuawa Julai 26 katika mashambulizi mengine ya muungano huo katika mji wa Raqqah, kaskazini mwa Syria.

Marekani katika miaka ya hivi karibuni imeua na kujeruhi makumi ya maelfu ya raia wa Syria na Iraq kwa kisingizio cha kupambana na magenge ya kigaidi katika nchi hizo.