Gallup: Wamarekani wengi wanataka Korea Kaskazini ishambuliwe kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i34403-gallup_wamarekani_wengi_wanataka_korea_kaskazini_ishambuliwe_kijeshi
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni na taasisi ya Gallup yanaonyesha kuwa, nusu ya wananchi wa Marekani wanaunga mkono suala la kushambulia kijeshi Korea Kaskazini.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 16, 2017 02:36 UTC
  • Gallup: Wamarekani wengi wanataka Korea Kaskazini ishambuliwe kijeshi

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni na taasisi ya Gallup yanaonyesha kuwa, nusu ya wananchi wa Marekani wanaunga mkono suala la kushambulia kijeshi Korea Kaskazini.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana Ijumaa inasema kuwa, asilimia 58 ya Wamarekani wanafadhilisha kutumiwa njia za kijeshi 'kuinyamazisha Pyongyang' iwapo jitihada za kiuchumi na kidiplomasia hazitazaa matunda.

Uchunguzi wa Gallup umebainisha kuwa, 86 ya wafuasi wa chama cha Republican wanaunga mkono kushambuliwa kijeshi Pyongyang, ikilingajnishwa na asilimia 37 ya wafuasi wa Democrats.

Kadhalika zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wa Marekani wamesema suala la Washington kuishambulia Korea Kaskazini katika muda wa miezi sita ijayo haliwezi kuepukika.

Kombora la balestiki la Korea Kaskazini

Matokeo ya utafiti huo yanatolewa katika hali ambayo, alfajiri ya jana, Korea Kaskazini ilivurumisha kombora jingine lililopaa juu ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido, kama radiamali ya kukosoa duru mpya ya vikwazo iliyopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Pyongyang.

Kabla ya jaribio hilo la jana, Korea Kaskazini ilitishia 'kuizamisha' Japan  na kuigeuza majivu Marekani.