Uamuzi wa Trump kuhusu Quds waendelea kupingwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i41423-uamuzi_wa_trump_kuhusu_quds_waendelea_kupingwa
Wimbi jipya la upinzani dhidi ya maamuzi ya viongozi wa Marekani wanaotaka kutambuliwa Quds (Jerusalem) kama mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, limechukua mkondo wake.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Mar 09, 2018 16:04 UTC
  • Uamuzi wa Trump kuhusu Quds waendelea kupingwa

Wimbi jipya la upinzani dhidi ya maamuzi ya viongozi wa Marekani wanaotaka kutambuliwa Quds (Jerusalem) kama mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, limechukua mkondo wake.

Federica Mogherini, Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya ameitaja hatua ya Marekani ya kutangaza wakati wa kuhamishwa ubalozi wa nchi hiyo kutoka Tel Aviv hadi Quds kuwa ni uamuzi wa kushangaza.

Federica Mogherini, Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya 

Mike Pence Makamu wa Rais wa Marekani Jumatatu usiku alisema katika kikao cha Kamati ya Uhusiano wa Umma kati ya Marekani na Israel (AIPAC) kuwa Washington imedhamiria kufungua ubalozi wake huko Quds kufikia mwezi Mei mwaka huu.  

Huku akipuuza upinzani wa jamii ya kimataifa kwa hatua hiyo ya Marekani Pence ameongeza kuwa Washington itaendelea kuwa pamoja na Israel. 

Kwa upande wake Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amekosoa uamuzi huo wa upande mmoja wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuitambua Quds kama mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa wakati wa kuitambua Quds kama mji mkuu wa Palestina utafika.