Waislamu Ufaransa walaani makala iliyopotosha Qur'ani tukufu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i43590-waislamu_ufaransa_walaani_makala_iliyopotosha_qur'ani_tukufu
Waislamu nchini Ufaransa wamelaani vikali kitendo cha kuchapishwa makala iliyovunjia heshima na kupotosha kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 24, 2018 11:59 UTC
  • Waislamu Ufaransa walaani makala iliyopotosha Qur'ani tukufu

Waislamu nchini Ufaransa wamelaani vikali kitendo cha kuchapishwa makala iliyovunjia heshima na kupotosha kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini humo.

Makala hiyo ya dharau na iliyo dhidi ya Uislamu ambayo imechapishwa hivi karibuni katika gazeti la Le Parisien mjini Paris, imesainiwa na rais wa zamani wa nchi hiyo, Nicolas Sarkozy, aliyekuwa waziri mkuu Manuel Valls na watu wengine 300.

Makala hiyo imetaka kufutwa baadhi ya Aya za kitabu kitakatifu cha Qur'ani kama ilivyosisitizwa na mwandishi wa makala hiyo, Pascal Bruckner.

Imam wa msikiti mkuu wa mji wa Bordeaux, Tariq Obroy amelaani vikali hatua hiyo inayohujumu Uislamu na kusema: Hatua hiyo inatokana na ufahamu usio sahihi na tafsiri potofu ya Qur'ani.

Hatua kama hizi za waandishi wa Magharibi za kuhujumu Uislamu na kitabu kitakatifu cha Qur'ani zimekuwa zikishuhudiwa mara kwa mara katika nchi za Ulaya. 

Miaka kadhaa iliyopita Salman Rushie wa Uingereza aliandika kitabu alichokipa jina la "Aya za Shetani" akihujumu matukufu ya Kiislamu kikiwemo kitabu kitakatifu cha Qur'ani. Vilevile gazeti la Charlie Hebdo na huko huko Ufaransa liliwahi kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).