Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake umekita mizizi katika sekta za elimu nchini Marekani
(last modified Thu, 14 Jun 2018 02:23:45 GMT )
Jun 14, 2018 02:23 UTC
  • Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake umekita mizizi katika sekta za elimu nchini Marekani

Matokeo mapya kabisa ya uchunguzi yanaonyesha kwamba, nusu ya wanawake wanaofanya kazi katika sekta za elimu na teknolojia nchini Marekani, wako katika hatari kubwa ya kubakwa na kudhalilishwa kijinsia.

Gazeti la Washington Post limeandika kuwa, uchunguzi unaonyesha kwamba unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake umeongezeka zaidi katika kumbi za mihadhara ya kielimu, maabara, ofisi na vituo mbalimbali vya kielimu, vituo vya mafunzo na hospitali za Marekani na kwamba, hata wataalamu wa kike wanakabiliwa na matatizo ya aina hiyo.

Jamii ya wasio wazungu ikihamasisha kampeni ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia

 Ripoti hiyo imefafanua kuwa, ushiriki wa wanawake katika shughuli za kielimu nchini Marekani unayaweka maisha yao matatani. Ripoti hiyo yenye kurasa 300 ambayo imetolewa na Kevin Savartot, mtafiti wa Chuo Kikuu cha jimbo la Georgia nchini Marekani, inaonyesha kwamba asilimia 20 hadi 50 ya wanafunzi wa kike katika sekta za elimu, teknolojia, uhandisi au udaktari na kutengeneza madawa katika vyuo vikuu vya Texas na Pennsylvania wamekumbwa na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Mmoja wa wanawake waliodhalilishwa kijinsia nchini Marekani

Aidha utafiti huo umeongeza kuwa wanawake wasiokuwa wazungu ndio wanaonyanyaswa zaidi na wafanyakazi wenzao wazungu na kwamba kutokana na ubaguzi wanaofanyiwa, wanajihisi kutokua na amani.

Hayo yanajiri katika hali ambayo Marekani bado inajitapa kuwa polisi wa dunia na mtetezi wa haki za wanawake.

Tags