Malalamiko ya Syria kutokana na kuendelea jinai za muungano vamizi wa Marekani
(last modified Mon, 07 Jan 2019 08:20:43 GMT )
Jan 07, 2019 08:20 UTC
  • Malalamiko ya Syria kutokana na kuendelea jinai za muungano vamizi wa Marekani

Kwa mara nyingine Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imewatumia barua mbili tofauti Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza la Usalama la umoja huo, ikilalamikia jinai zinazofanywa na muungano vamizi unaojiita eti dhidi ya Daesh (ISIS) unaoongozwa na Marekani huko katika jimbo la Deir ez-Zor nchini humo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, ndege za muungano huo vamizi zilifanya mashambulizi ya kinyama katika jimbo la Deir ez-Zor ambayo yameua raia 21 wakiwemo watoto wadogo. Tangu mwezi Agosti 2014, Marekani na nchi washirika wake na kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh bila ya idhini ya Umoja wa Mataifa wala ruhusa ya serikali ya sasa ya Syria, iliunda muungano wa kile ilichokiita kuwa ni wa kimataifa na hadi sasa muungano huuo umefanya mauaji ya raia wengi wasio na hatia wa nchi hiyo. Suala hilo limekuwa likipingwa sana na fikra za walio wengi ndani na nje ya Syria. Kuendelea jinai za Marekani kunafanyika katika hali ambayo Rais Donald Trump wa Marekani na kutokana na kushindwa nchi yake huko Syria, hivi karibuni alitangaza maamuzi ya kimaonyesho tuu ya kuondoka askari wa Marekani katika ardhi ya nchi hiyo ya Kiarabu, maamuzi ambayo yametajwa kuwa ni kukimbia askari hao vamizi.

Hujuma za kinyama za ndege za Marekani nchini Syria

Wiki kadhaa  baada ya kutangazwa uamuzi huo Trump amebadili sera na maamuzi yake ya awali na sasa ametangaza kuwa askari wa nchi hiyo wataondoka kwa awamu na hatua kwa hatua katika ardhi ya Syria. Harakati hii imefuchufua masuala ya nyuma ya pazia na maamuzi ya kushtukiza, ya kimaonyesho na hata yanayogongana na Donald Trump kuhusiana na Syria. Kupitia siasa hizo za kimaonyesho, Trump anakusudia sambamba na kupunguza malalamiko ya fikra za walio wengi kuhusiana na jinai za nchi yake katika eneo la Mashariki ya Kati, aweze pia kuanadaa mazingira ya kutupilia mbali maamuzi hayo katika siku za usoni kwa kutumia visingizio mbalimbali.  Siasa kama hizo yaani za kuzishughulisha fikra za walimwengu kupitia hatua za kimaonyesho za Rais huyo wa Marekani, matokeo yake ni kuzidisha jinai zilizoratibiwa na Washington nchini Syria. Kuongezeka kiwango cha mauaji ya raia wa Syria kunakotokana na harakati za muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Marekani kunaakisi suala hilo na hatari ya siasa za Trump kwa jamii ya kimataifa.

Magaidi wa Daesh (ISIS) ambao wanatumiwa na Magharibi kwa ajili ya kuhalalisha uvamizi wao kwa nchi za Waislamu

Katika uwanja huo, gazeti la Al-Thawra la Syria na kupitia uchambuzi wake kuhusu suala hilo limeandika kwamba: "Kwa mara nyingine serikali ya Trump inafanya upotoshaji na kusambaza habari zenye mgongano ambapo kwa upande mmoja zinaeleza kuondoka haraka  askari wa nchi hiyo kutoka Syria, na upande mwingine zinachelewesha na kurefusha kipindi cha kuondoka askari hao katika nchi hiyo ya Kiarabu." Ukweli ni kwamba Marekani imefeli na imetumbukia kabisa katika kinamasi katika kipindi cha Rais Donald Trump. Mchambuzi Ahmed Hamada anasema: "Washington inadai kupambana na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) katika hali ambayo ni Marekani hiyo hiyo ndio inafanya njama mbalimbali kwa ajili ya kulibakisha hai kundi hilo. 

Tags